RC MAKALLA AONGOZA HARAMBEE YA KUICHANGIA PAMBA JIJI FC, ZAIDI YA MILIONI 177 ZAPATIKANA
*Awashukuru wachangiaji kwa kufanikisha harambee*
*Ahimiza kuipa nguvu ya kiuchumi Pamba FC kwa kununua jezi kwa wingi*
*Awahakikishia wana Mwanza fedha zitakuwa salama*
*Abainisha Mkakati wa kuipandisha timu hiyo Ligi kuu*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Februari 11, 2024 amewaongoza Wana Mwanza na wadau wa michezo katika harambee ya kuichangia timu ya soka ya Pamba Jiji FC na kufanikisha kukusanya jumla ya Shilongi milioni 177.3
Harambee hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwanza Hotel michango hiyo imetoka kwa watu, taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi wameitikia kwa wingi zoezi hilo lenye lengo la kuipa nguvu Pamba FC katika michezo yake ya Ligi ya Championship ili ipande kwenda Ligi kuu.
Katika hotuba yake ya kuwashukuru waliofanikisha harambee hiyo Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ni mlezi wa timu hiyo maarufu kama TP Lindanda amebainisha kuwa kupanda Ligi kuu siyo lele mama bali ni lazima kuwe na mikakati ya uhakika wa kifedha ambayo ndiyo chanzo cha mafanikio.
"Nilipoingia rasmi kama Mkuu wa Mkoa huu niliichunguza Pamba FC na kubaini inahitaji haraka nguvu ya kifedha, wameingia ndugu zetu wa NetSports hatuna budi kununua jezi kwa wingi ili kuzidi kuimarisha kiuchumi timu hii", CPA Makalla
Hotuba hiyo ya Mkuu wa Mkoa iliwaongezea hamasa washiriki wa harambee hiyo na kuzinunua kwa wingi jezi za Pamba Jiji wakiongizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe. Michael Masanja.
"Ndugu mgeni rasmi Mkuu wetu wa Mkoa hizi jitihada zako sisi kama viongozi wa soka Mkoa zinazidi kutupa ari kuwa mstari wa mbele kuipigania Pamba Jiji FC ili ifike malengo ya kupanda Ligi kuu msimu ujao," Vedasto Lugano M/kiti MZFA.
Meya wa Jiji la Mwanza ambaye ni wamiliki wa Pamba Jiji FC Mhe. Costantine Sima amebainisha watahakikisha nguvu hiyo ya wadau haipotei bure bali utakuja na matokeo chanya ambayo ni kucheza Ligi kuu msimu ujao.
Fedha hizo zilizotokana na harambee ni pamoja na michango taslimu ambayo ni zaidi ya Shilingi Milioni 28 na ahadi zaidi ya Shilingi milioni 100.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.