RC MAKALLA ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA KUPOKEA WATOTO SHULENI ILEMELA
*Awapongeza jinsi wamejipanga kupokea wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza*
*Atoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwani*
*Agawa uji na kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kutimiza ndoto zao*
*Wanafunzi wamshukuru Rais Samia kwa elimu bila malipo na kuwajengea miundombinu bora*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewapongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu tayari kwa kupokea wanafunzi kwa muhula mpya wa masomo 2024 ulioanza jana nchini.
Ametoa pongezi hizo mapema leo Januari 09, 2024 wilayani Ilemela akiwa ziarani kukagua namna walivyojipanga kupokea wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na Kidato cha kwanza kwa ukaguzi wa miundombinu na namna wanafunzi wanavyoendelea kuripoti.
Akiwa kwenye shule ya ufundi ya wavulana Bwiru ambapo ameshiriki zoezi la kugawa uji kwa wanafunzi Makalla amesema Ilemela wamejipanga vyema kwani tayari wana madarasa, matundu ya vyoo, viti na meza vinavyotosha kupokea watoto 150 wapya shuleni hapo.
Katika nyakati tofauti akiwa anazungumza na wanafunzi wa Sekondari na Msingi, Makalla ametoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule huku akibainisha kuwa hakuna ada wanayotakiwa kupeleka hivyo ni wajibu wao kuhakikisha watoto wanapata elimu.
"Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu, tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea madarasa mazuri hakuna mwanafunzi anayekaa chini na viti na madarasa ni mazuri." Amesema Zaujath Najim, mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Kisenga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.