RC MAKALLA AWAKARIBISHA INDONESIA KUWEKEZA MAZAO YA NGOZI NA MADINI
*Asema Mwanza ina maeneo mengi yenye fursa za uwekezaji ukiwemo uvuvi
*Apongeza uhusiano wa Tanzania na Indonesia ulioanza tangu mwaka 1964
*Asema makubaliano ya mashirikiano yaliyofanywa na Marais yataongeza tija ya Maendeleo*
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo amefanya mazungumzo mafupi na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe.Tri Yogo Jatmiko na kutoa fursa ya kuwekeza katika mazao ya ngozi na madini yanayopatikana kwa wingi mkoani humo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa yakijumuisha maafisa kutoka ubalozi huo na mwakilishi kutoka Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkuu huyo wa mkoa amesema makubaliano ya mashirikiano yaliyofanywa na viongozi wa Mataifa hayo hivi karibuni ni lazima yawe na matokeo chanya kama uwekezaji huo.
"Mhe Rais wetu alifanya ziara hivi karibuni nchini Indonesia na kuingia makubaliano ya mashirikiano katika sekta mbalimbali kama elimu,kilimo,afya na biashara,lakini pia hapa mkoani kwetu zipo fursa nyingi ambazo zikipata mwekezaji zitakuwa na tija kwa wananchi wa pande zote mbili,"CPA Makalla
Amebainisha nchi ya Indonesia tuliyoingia nayo mahusiano tangu mwaka 1964 ni wazalishaji wakubwa wa mafuta ya mawese ambayo waliyatoa hapa nchini kwetu, wamewekeza zao la karafuu huko Zanzibar na sasa wanataka kujikita kwenye zao la Tangawizi,hii yote ni faida ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo.
Aisha ameipongeza Indonesia kwa kuwajengea uwezo wataalam wa chuo cha DIT hali ambayo itaongeza tija Katika uzalishaji bora wa mazao ya ngozi.
Naye Balozi wa Indonesia Tri Yogo Jatmiko amesema anatekeleza na kuimarisha makubaliano yaliyowekwa baina ya nchi ya Indonesia na Tanzania katika sekta mbalimbali.
Indonesia imeanza kutoa mafunzo kwa wataalam wa ngozi kwenye chuo cha DIT kuanzia leo hadi Machi 8 2024 na mafunzo hayo yatakuwa yakifanyika kwa awamu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.