RC MAKALLA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masalla amewakaribisha wafanyabiashara kuchangamkia fursa za uwekezaji mkoani Mwanza kutokana na kuwepo na mazingira rafiki ya kuwekeza.
Akizungumza leo Novemba 3, 2023 kwa niaba ya Mkuu wa Mko kwenye kongamano la kibiashara la Jiongeze lililoandaliwa na Kampuni ya Wasafi, Mhe.Masalla amesema kukamilika kwa miradi ya kimkakati ikiwemo Reli ya kisasa SGR,Daraja la JP Magufuli na Meli ya abiria ya Mv Mwanza zitachangia kurahisisha shughuli zote za kibiashara.
"Mwanza tuna rasilimali kubwa ya Ziwa Victoria kunakofanyika shughuli za uvuvi wa samaki na dagaa utakapo wekeza eneo hili utakuwa na uhakika wa kipato kutokana na miundombinu ya usafirishaji kuwa rafiki iwe barabara,ndege au njia ya reli,"amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza na washiriki wa kongamano hilo.
Ameongeza kuwa wafanyabiashara wengi walishindwa kusafirisha mizigo yao kwa ukubwa lakini kuwepo kwa mradi wa reli ya kisasa na uwepo wa Meli uhakika wa kusafirisha mizigo kwa usalama na kwa wingi sasa hakuna shaka.
Awali akitoa utangulizi wa taarifa za fursa za uwekezaji Mwanza,Katibu Tawala wa Mkoa huo,Ndg.Balandya Elikana amebainisha Mkoa huo kuwa karibu na eneo la nchi za maziwa makuu ni fursa pekee ya kiuchumi kutokana na mazingira rafiki ya miundombinu ya usafiri.
"Ukuaji wa kiuchumi wa Mkoa wa Mwanza ni lazima sasa bidhaa nyingi zipatikane hapa tofauti na wengi kukimbilia Kariakoo,uwanja wetu wa ndege upo mbioni kukamilika na kuwa wa kimataifa Utalii utakuwa na tija kutokana na ukaribu wa Mwanza na mbuga ya Serengeti ambao ni mwendo wa saa mbili na nusu,"Balandya.
Kongamano hilo lililokuwa na utoaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Taasisi za Serikali,washiriki walipata fursa ya kujua ufugaji wa kisasa wa ng'ombe aina ya Borani.
"Tuna shamba letu la Taifa la Mabuki huko sasa hivi kunaendelea mradi wa utoaji elimu kwa vijana namna ya ufugaji wa ng'ombe kwa tija ikiwemo utoaji maziwa kwa wingi na unenepeshaji wa kuwa na kilo zaidi ya 200",Peter Kasele,Afisa mifugo.
"Mkoa wa Mwanza alisilimia 53 ni maji ya ziwa Victoria hivyo kilimo cha umwagiliaji kina nafasi kubwa,mazao ya jamii ya mikunde,mahindi pia mpunga kina stawi sana,"Innocent Keya, Afisa kilimo.
"Tuna vivutio vingi vya Utalii Mkoani Mwanza,kuanzia mbuga ya Sanane,makumbusho ya mila za kabila la wasukuma ya Bujora pamoja na Utalii ndani ya Ziwa Victoria hasa uwepo wa jiwe la Bismark,"Gloria Mnihambo,Afisa bodi ya Utalii.
Kongamano hilo limewajumuisha zaidi ya washiriki 200 kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara,wadau wa sekta ya Utalii,pamoja na wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo vikuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.