RC MAKALLA AWAPONGEZA BUSOLWA MINING KAMPUNI YA UCHIMBAJI WA MADINI ISHOKELA- MISUNGWI
Asifu Uwekezaji Mgodi wa Kisasa na uzingatiaji wa Sheria za Kisekta*
Amewaagiza TANESCO, RUWASA na TARURA kuboresha huduma kwenye Migodi*
Awapongeza kwa kutoa huduma za kijamii kwa wakazi wanaozunguka Mgodi*
Ametoa wito kwa wawekezaji hao kuuza Madini yao kwenye Masoko rasmi*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amezipongeza Kampuni za Kizawa za Uchimbaji Madini za Busolwa Mining Com LTD na Isinka Federation kwa Kuwekeza zaidi ya Bilioni 37 kwenye Mradi wa Uchimbaji Madini unaotumia Teknolojia ya Kisasa ambapo umekua kinara kusaidia jamii inayozunguka mgodi huo kupitia huduma za Kijamii.
Ametoa pongezi hizo leo tarehe 14 Agosti, 2023 kwenye Kitongoji cha Ishokela kilichopo katika kijiji na Kata ya Buhunda wakati azikungumza na Wafanyakazi wa Mgodi wa Kampuni ya Busolwa Mining Co. LTD ja Mshirika wake wanaojishughulisha na Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu akiwa katika ziara ya Ukaguzi wa shughuli za Maendeleo Wilayani Misungwi.
"Hatujasikia Mgoogoro na wafanyakazi hapa nadhani inatokana kuwatimizia matakwa ya kisheria na ushirikiano mlionao kwa wananchi wanaowazunguka linatia faraja maana nimesikia mmetoa pia ajira zaidi ya 160 wa watanzania wenzenu jambo hili linaonesha mnawajali na mmewagusa kwenye kuwainua uchumi." Makalla.
Aidha, amebainisha kuwa kitendo cha Wawekezaji hao kuchangia zaidi ya Bilioni 5.3 Serikalini kupitia leseni na vibali mbalimbali ni uzalendo mkubwa na ametumia wasaa huo kuwataka Mamlaka zinazohusika na Usambazaji Maji, Nishati ya Umeme, na Miundombinu ya barabara kuharakisha huduma kwenye eneo hilo ili wawwkezaji hao wafanya kazi kwa amani.
"Nawashukuru Busolwa Mining Ltd na washirika wenu, nimeridhika na huduma mnazotoa, nimewaagiza timu ya wataalamu kutoka TANESCO Mkoa na Wilaya waje kushirikiana na wataalamu wenu hapa ili kutatua changamoto ya umeme mdogo na naahidi changamoto zote hizi zitakwisha na TARURA na TANROADS nimewaagiza pia kutatua suala la Usafiri."CPA Makalla.
Naye, Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Godfrey Sanga ametumia wasaa huo kuahidi kuwa Ifikapo Novemba Mwaka huu kampuni hizo zitapata Maji ya kutosha kwani kuna Mradi wa kuzalisha Ita Milioni Tano kwa Siku unaoendelea kujengwa na kwamba tayari Tangi limeshajengwa kwenye Mlima jirani na Mgodu huo.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa kwenye maeneo mengine ya Migodi tumekua tukisikia hili ma lile lakini kwa hawa Busolwa Mining Co. Ltd hatujapokea taarifa ya Mgogoro wa Kiutumishi, Maslahi kwa watumishi, kukwepa Kodi za Serikali wala matatizo ya Kimazingira na kwakweli nawapongeza sana." Amesema Paulo Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.
Ndugu Masumbuko Thobias, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Mgodi huo ameeleza kuwa Mgodi unamilikiwa kwa Ubia baina ya Kampuni Mbili kwa Leseni namba 555 ya Mwaka 2015 na kwamba wanafanya uchimbaji wa Kisasa wa Wazi na wanawajengea uwezo wachimbaji wadogo ili kuwainua kiuchumi.
Aidha, amefafanua kuwa gharama za Mradi huo ni zaidi ya Bilioni 37 na kwamba tangia waanze uzalishaji wamechangia zaidi ya Bilioni 5.3 kwenye Pato la Taifa kupitia mambo kadhaa kama Ushuru wa huduma, Kibali cha Usalama, Kodi ya uendeshaji, Ushuru wa bidhaa na ajira rasmi ambapo kwa pamoja vinasaidia kukuza uchumi wa nchi.
"Changamoto kubwa iliyopo hapa ni upatikanaji wa umeme wa uhakika, kumekuwepo na umeme mdogo unaosababisha kuunguza mitambo na inasababisha kutofikia malengo ya Mwezi lakini pia tuna tatizo la Maji na Barabara ambapo tunaamini ujio wako Mhe. Mkuu wa Mkoa utasaidia kututatulia adha hizi." Amefafanua Thobias.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.