RC MAKALLA AWATAKA WADAU WA MICHEZO MWANZA KUSHIRIKIANA KUPANDISHA TIMU LIGI KUU
*Asema Mpira hauna itikadi unawaleta watu pamoja*
*Asema mkakati ni Pamba Jiji ipande Ligi Kuu msimu huu, Mapinduzi FC ipande Championship*
*Alliance FC nayo isalie First League huku Copco ikipiganiwa isishuke daraja kutoka Championship*
*Aitisha hafla ya Kutunisha mfuko wa kusaidia timu zilizo katika ligi*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewataka viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani humo (MZFA) kuimarisha ushirikiano na timu za mpira wa miguu zilizoko kwenye ligi mbalimbali ili zipande daraja.
Ametoa wito huo leo januari 17, 2024 katika mkutano wake na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa huo pamoja na viongozi wa timu za Copco na Pamba Jiji zinazoshiriki Championship pamoja na Mapinduzi iliyo kwenye First League.
"Michezo ni uchumi, Mpira ni Uchumi kwani tukiwa na timu kwenye Ligi kuu basi Mkoa utafanya biashara mbalimbali hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na timu ya ligi kuu mkoani hapa na zingine kutoka madaraja ya chini zipande na kuja kwenye ligi za juu."
Makalla amesema kuwa michezo haina itikadi hivyo ni lazima wawe kitu kimoja katika kuhakikisha wanazipigania timu zote ili zipande kwenda ligi kuu na sio kuweka mahaba na ushabiki kwenye timu moja ambayo kwa muda mrefu imekua ikiugharimu mpira wa Mwanza.
Akizungumzia timu ya Pamba Jiji iliyoshuka kutoka Ligi Kuu mwaka 1992, amesema ni lazima ipande kutoka Championship ambapo wapo nafasi ya 2 kwa point 37 kwenda Ligi Kuu huku akitoa wito kwa Copco FC kuhakikisha wanabaki kwenye ligi hiyo halikadhalika Mapinduzi FC kuhakikisha wanapanda Championship kutoka First League ambako wako nafasi ya 1.
Aidha, ametumia wasaa huo kuwasihi wadau, makampuni na mashabiki wa mpira wa miguu mkoani humo kushirikiana kuhakikisha wanazisapoti timu zao kwa kuwatia moyo kwenye shida na raha hususani kwenye uwekezaji na sio kubaki wakilaumu tu wakati zinapofanya vibaya badala yake wawasapoti.
"Timu zote nawasihi tusiwe sehemu ya kuhujumiana badala yake tuwe kwa ajili ya kusaidiana, haifai kabisa ni lazima tuwe na uchungu wa kuhakikisha timu zetu zote Mkoa wa Mwanza zinapanda kutoka ligi ya chini kwenda ya juu hadi turudishe makali yetu Ligi kuu." Makalla.
Halikadhalika, Mkuu wa Mkoa ametoa kitita cha Milioni 6 yaani milioni 2 kwa kila timu katika kuwaunga mkono na kusaidia kushajihisha na kuwatia moyo kwenye safari yao ya kimpira inayoendelea ambazo amewataka wakazitumia katika kujikimu na mahitaji.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa huo Leonard Malongo ametumia wasaa huo kumhakikishia Mkuu wa Mkoa kushirikiana kubakikisha Mwanza inapata Timu kwenye Ligi kuu na kwamba watakua bega kwa bega kushirikiana na
Mwenyekiti wa Copco FC, Simon Romli amesema pamoja na mapambano mazito kwenye Ligi wao wanamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa mchango na upendo wake kwa mpira wa Mwanza na ameahidi kuwa watahakikisha wanashirikiana kuhakikisha Mwanza inakua ni mkoa wa Mpira kwa kuwa na timu kwenye Ligi kuu.
"Hakuna siku ambayo sitaisahau kama siku uliyoangalia mpira wa timu yetu tukiwa tumekaa pamoja kwenye mawe, unajali unawiwa na unakiu ya kupata timu kwenye Ligi kuu, tunakushukuru sana Mhe. Mkuu wa Mkoa." Mwenyekiti wa Pamba Bhiku Kotecha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.