RC MAKALLA : UGENI WA BALOZI WA ETHIOPIA MWANZA NI KUANGALIA MAENEO MBALIMBALI YA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
*Ni ziara ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia*
*Mwanza zipo fursa mbalimbali za kiuchumi likiwemo Ziwa Victoria*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amesema ujio wa Balozi wa Ethiopia Mkoani humo, Mhe Shibru Mamo utazidi kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na Ethiopia kutokana na Mwanza kuwa na fursa nyingi za kiuchumi likiwemo Ziwa Victoria.
Akizungumzia ujio wa Balozi huyo Ofisini kwake leo mara baada ya mazungumzo yao, Mkuu huo wa Mkoa amesema Ziwa Victoria kuna mazalia mengi ya samaki ambayo Balozi huyo atapata fursa ya kuona eneo lipi litakuwa mwafaka kiuchumi baina ya nchi hizo.
"Mnafahamu wenzetu wanaongoza kwa Ufugaji wa Ng'ombe Barani Afrika, na sisi ukanda huu tuna ufugaji pia hivyo tunaweza kubadilishana uzoefu katika eneo hilo pia Chuo Kikuu cha SAUT ni sehemu nzuri ya kubadilishana uzoefu wa mipango ya vyuo",-CPA Makalla
"Nimefarijika kufika hapa Mwanza na nitatembelea maeneo ya Chuo Kikuu cha SAUT, Uhamiaji na Gereza la Butimba,yapo mambo nitakayojifunza ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zetu", Mhe.Balozi Shibru Mamo.
Ziara hiyo ya Balozi wa Ethiopia ni msisitizo wa ushirikiano aliosema Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu alipofanya ziara nchini
Ethiopia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.