*RC Malima ahimiza ushirikiano wa kimaendeleo na viongozi wa Kimila Mwanza
Viongozi wa Kimila wa Mkoani Mwanza wameombwa kuushirikisha uongozi wa Mkoa katika kazi zao pamoja na mambo ambayo yakipata ushirikiano wa Uongozi yanaweza kuleta maendeleo katika Mkoa huo.
Wito huo umetolewa leo Mei 11, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima wakati alipokutana na Viongozi wa Kimila wa Mkoani humo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
" Kama yapo mambo ambayo yanahusiana na mafanikio katika kazi zenu basi naomba mnishirikishe hata katika mambo yote ambayo yanaweza kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa watu wa Mwanza na kanda ya Ziwa kwa ujumla," RC Malima
Aidha Mhe. Malima ameongeza kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na Chuo cha Mt. Augustino (SAUT) wanampango wa kuanzisha (Kituo cha Ubunifu cha Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia) ili kiweze kuwasadia wananchi wa Mkoa huo.
Serikali ya Mkoa imeamua kufanya kampeni mahususi ili kujaribu kuwafikia wananchi wake kwahiyo kuna kituo cha kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi( Kituo cha Ubunifu cha Maendeleo na Sayansi na Teknolojia) ambacho tunataka tukianzishe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino (SAUT)," Amesema Mkuu huyo wa Mkoa
Naye Mtemi. Charles Itale wa kwanza wa Bujashi Magu na Mwenyekiti wa Umoja wa Watemi Mkoa wa Mwanza ameongeza kiwa kitu kinachosababisha mmomonyoko wa maadili ni kuchukulia swala la malezi kama jukumu la mtu mmoja na sio la jamii kwa ujumla jambo ambalo linaleta utofauti na zamani
Pia Mtemi. Domina Musiba wa Tatu wa Buchosa amewaomba viongozi wa kiserikali na wa kidini waweze kusimamia maswala ya kimaadili na pia wapate wasaa wa kuielimisha jamii pale wanapokutana nayo ili waweze kurudisha maadili kama kipindi cha zamani
"Tunaomba sana viongozi wote wa dini hata wa Serikali wanapokutana na wananchi waweze kusimama na kutoa elimu kuhusu mambo ya maadili kwa jamii na pia wajenge uhusiano mzuri na Watemi ili tuweze kukutane na kuuzungumza kuhusu maadili na mienendo ya jamii zetu kwa ujumla.
Mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na viongozi wa kimila ulilenga kujadili maswala ya mmomonyoko wa maadili katika jamii na kujadili juu ya tamasha la bulabo ambalo ni maalum kwa ajili ya kusherehekea mavuno kwa mila za kabila la Kisukuma ambazo zitafanyika Juni 11 hadi 17 2023 katika kata ya kisesa wilaya ya Magu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.