Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka waratibu wa Mashindano ya Mitumbwi kuongeza ubunifu ktk mchezo huo ili kuwapatia washiriki bora watakaomudu ushindani wa kimataifa.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita Mwaloni Kirumba kwa niaba yake, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala amesema michezo ukiwemo huo wa Mitumbwi imekuwa nguzo imara ya ajira na kuwafanya wanamichezo kuwa na kipato kikubwa hivyo kuna kila sababu ya kuwajengea mazingira ya kisasa wanamichezo hao kuwa wa kimataifa.
"Nawapa Rai waandaaji wa Mashindano haya ambayo yanafanyika kila mwaka hapa Mwanza,hawa wanazofanya vizuri wasiishie kuwapa zawadi ya pesa tu na kuja kuwatafuta mashindano yajayo hii ni sawa na kutoutendea haki mchezo huu na wachezaji husika Mhe.Masala.
Amesema mashindano haya sasa huu ni mwaka wa 14 tangu yaanzishwe,waandaaji sasa muone kuna kila sababu ya kuyatoa nje ya mipaka yetu ambapo huko hawa wachezaji watazidi kupata fursa ya ushindani wa juu na kupata timu za kulipwa ambayo ndiyo yawe malengo yetu na siyo kuishia hapa hapa tu.
Aidha amewapongeza waandaaji hao kwa kuzidi kuupa hamasa mchezo huo kiasi cha kuwa na mvuto kwa wakazi wa Mwanza na kutoa nafasi ya kuutangaza Mkoa huo Vivutio vingi vyenye fursa mbalimbali ikiwemo rasilimali ya maji ya Ziwa Victoria.
Naye msimamizi wa bodi ya Utalii Kanda ya Ziwa Gloria Muhambo amewahakikishia washiriki wa mchezo huo kuzidi kupewa ushirikiano kutokana na mashindano hayo kutoa ujumbe wa Vivutio vya Kitalii vilivyopo ndani ya Mkoa wa Mwanza.
"Tumeshuhudia uwezo mzuri wa kupiga makasia kwa washiriki wanaume na wanawake,naamini tutakapo wapa fursa ya ushiriki wa kimataifa Mkoa wetu utazidi kung'ara.
"Mkakati wetu sasa na kuyashirikisha Mataifa ya ukanda wa Maziwa Makuu kuwashindanisha wanamichezo wetu lengo likiwa ni kuwafungulia fursa za kuchomoza Kimataifa" Ludovick Kanyebuye mratibu wa mashindano ya mitumbwi Mkoa wa Mwanza.
Naye mratibu wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya SCOPE inayosimamia mashindano hayo Benard Mweta amebainisha wamejipanga kuhakikisha mashindano yanakuwa bora na kuzidi kuviinua na kuvikuza vipaji vya washiriki ili waje kuwa washindani wa kimataifa
Katika mashindano hayo timu za kutoka Misungwi zimetoka kimaso maso kwa wanaume na wanawake kutokana na kushika nafasi za kwanza hadi tano,ambapo mahindi wa wanza amekunja kitita cha Shs milioni mbili,wa pili milioni moja na nusu,wa tatu milioni moja huku mshindi wa nne akitoka na laki 8 na wa tano akipata laki 5
Mashindano hayo yameshirikisha jumla ya timu 78,Wanawake wakiwa 18 kutoka Mara,Ukerewe,Misungwi na wenyeji Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.