Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima akiwa ziarani Wilayani Sengerema ameitembelea Kambi ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana kwa siku tatu katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi wakipeana mafunzo ya Itifaki na uzalendo.
Mhe. Malima ametoa wito kwa vijana hao pamoja na mambo mengine kuwa na kanzidata ili iwepo takwimu sahihi ya wanachama huku akibanisha kuwa mikakati ya kutimiza dira ya uhakika wa kupata Ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu na chaguzi zingine itatokana na kuwa na takwimu sahihi za wananchama katika kila kundi.
"Uimara wa Chama Cha Mapinduzi haujaja hivi hivi, ni maandalizi mazuri ya waasisi na viongozi kwa vijana katika kuwajengea Misingi ya kulitumikia Taifa lao kizalendo na ndio maana kijana wa hiki popote utapomkuta utambaini kwa nidhamu yake kubwa katika kukisemea chama chake." Mhe. Malima amesisitiza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema Ndg. Makoe Augustino ametoa wito kwa vijana hao kushirikiana na serikali na Chama Cha Mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo lakini pia waendelee kujibidiisha kwenye masomo na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mwanza Ndg Chrisrian Kimaro ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Bugando ametumia wasaa huo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani kwa ufanisi mkubwa huku akitolea mfano miradi ya kimkakati kama daraja la Kigongo Busisi ambalo litakapokamilika litachochea uchumi wa kanda ya ziwa.
Vilevile, amempongeza Mwenyekiti Taifa kwa kuisimamia vema Serikali ya awamu ya Sita hasa kwa upande wao kwani pamoja na uboreshaji wa mambo mengine, fedha za Mikopo zimetolewa kwa wanafunzi kwa ufanisi kwani siku za karibuni wameweza kupokea hadi duru la nane jambo ambalo ni tofauti na miaka mingine ambapo kwa wakati huu ingetoka duru la sita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.