Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewahimiza Wananchi Mkoani humo kuelimika vya kutosha na kuchangamkia mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao ni Mkombozi kwa Mtanzania.
Akizungumza leo na wawakilishi wa makundi mbalimbali kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kuelimishana kuhusiana na mfumo huo mpya unaokuja, Mhe. Malima amesema Muswada huo baada ya kuwa Sheria na kupitishwa na Bunge ni jukumu la kila mwananchi kupata huduma hiyo.
"Nina kila sababu ya kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameimarisha miundombinu ya Sekta ya Afya ambapo mwananchi sasa hapati usumbufu wa kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo". Amesema Mhe. Malima.
Amesema siku zote ugonjwa haubishi hodi na mfumo huu wa Bima kwa wote unatumika duniani kote na Tanzania imepiga hatua nzuri tofauti na Mataifa yaliyoendelea ambayo yamekutana na changamoto kadhaa.
"Watanzania wana kila sababu ya kuchangamkia fursa hii ambayo itamgusa kila mtu hata asiye na uwezo kwani Serikali itakuwa ikitenga kila mwaka Shs Bilioni 359 kwa ajili ya wale wasio na uwezo kupata huduma hii na Shs Bilioni 149 kwa wale watakaoingia wakati mfumo unaendelea na hawana uwezo". Emmanuel Mwikabwe Meneja wa Mfuko wa Bima.
"Wanachana wa Mfuko wa Bima wa CHIF wataendelea kuwa hai hadi mwisho wa mwaka uanachama wao utakapo Kona na wataingia kwenye mfumo huu mpya". Dkt.Bahati Msaki, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Ture.
Mkutano huo wa kuelimishana umewakutanisha Wakuu wa Wilaya zote, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, wawakilishi wa viongozi wa Dini, Wafanya biashara ndogo ndogo na viongozi wa Sekta ya usafirishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.