Leo Septemba 15, 2022 Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Joachim Otaru kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, amezindua Tawi la Kampuni ya Alpha Associates (T) Limited Mkoani humo kwenye hafla iliyoenda Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 22 ya Kampuni hiyo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Nyanza jijini humo, Ndugu Otaru ametoa wito kwa makampuni binafsi, umma na taasisi mkoani humo kupata msaada kwa huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ambayo kwa uwepo wa tawi hilo itakua jirani.
"Nitumie fursa hii kukupongeza sana Dkt. Massaga kwa kuamua kuja kufungua tawi hapa Mwanza na naomba uzoefu mlioutumia kwenye mikoa mingine muutumie kunufaisha makampuni ya hapa Mwanza hasa kwenye nyanja za TEHAMA na ufanyaji wa biashara kwa mfuko rahisi wa kisasa" Amesema, Otaru.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alpha Associates Tanzania Limited Dkt. Alphonce Massaga ametumia siku hiyo adhimu kuwashukuru wafanyakazi kwa ushirikiano, umoja na upendo uliofanikisha ufanisi wa kampuni hiyo kwa kipindi chote cha uhai wa Kampuni.
"Mafanikio yoyote yanaaza kwenye kuthubutu na kuamua kulifanyia kazi wazo lako, kuamini na baadae kuamua kulifanyia kazi wazo lako na kwakweli kwa kupitia maandiko na makongamano mbalimbali yalinijenga na kunifanya leo kufikia hapa kupitia kampuni hii." Amesema Dkt. Massaga wakati akitoa neno la kutokata tamaa.
Mkuu wa Kitengo cha Ushauri kwenye kampuni hiyo, CPA Dalali Njire ametumia wasaa huo kuyakaribisha makampuni kupata huduma kwenye tawi hilo huku akibainisha kuwa kampuni hiyo inatoa huduma za Ushauri wa masuala ya Kodi, huduma za Kihasibu, kukaguliwa masuala ya kifedha na hesabu za mwisho na huduma za sheria.
Awali, Meneja wa Utumishi na Rasilimaliwatu Bi. Anna Zakayo alifafanua kuwa kwa kipindi cha Miaka 22 ya uhai wa Kampuni hiyo wanajivunia kwa kuongoza Ofisi kwa Sera bora kwenye idara mbalimbali za kodi, usalama na utawala kama vile kuajiri na kuhudumia watumishi wao kwa kufuata sheria na miongozo ya nchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.