Mkoa wa Mwanza umetoa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo (Machinga) na watoa huduma wadogo elfu 73,000 kwa awamu ya pili mwaka huu,kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Wilaya zote .
Ambapo awamu ya kwanza walikabidhiwa vitambulisho 15,000 vya wafanyabiashara wadogo (Machinga ) vyenye thamani ya million 300 ambapo vilivyogawiwa ni 7,792 sawa na asilimia 51.95 huku vitambulisho 7,208 sawa na asilimia 48.05 vikiendelea kugawiwa na kiasi cha fedha cha milioni 155.84 (Tsh.155,840,000) zikiwasilishwa TRA.
Akizungumza wakati akiwakabidhi vitambulisho hivyokutoka ofisi ya Rais Tamisemi vilivyopitia Mamlaka ya Mapato Tanzania “TRA” Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella aliwataka viongozi hao kuhakikisha fedha zote zinakwenda benki
Anasema jumla ya vitambulisho vilivyopokewa Mkoa wa Mwanza ni 88,000 vyenye thamani ya billion 1.76, hivyo hadi sasa kwa awamu ya kwanza wameuza kwa asilimia 54 na amewataka kuhakikisha zoezi hilo wanalifunga ndani ya wiki moja pia waratibu wawe makini kwa sababu mfumo umeboreshwa na unafanyakazi ipasavyo hivyo kula hela ya serikali haiwezekani.
" Vitambulisho ni Jambo vyeti sana hivyo tulitilie mkazo vinaweza kukupotezea mwelekeo kwa ushauri wangu vitambulisho hivi tulivyowagawia awamu ya pili tuvimalize mwezi wa nane "anasema Mongella.
Anasema vitambulisho visikae Halmashauri bali vifike kila sehemu kwa sababu Mhe.Dkt. Rais Magufuli alitoa ahadi kwa wananchi kuhusiana na vitambulisho hivyo, ni wakati wa kufanya kazi ili kuleta matokeo yanayoonekana.
" Ninawapongeza Magu, Kwimba na Misungwi kwa kuanzia wamefanya kazi nzuri na wameonyesha njia kufikia leo jioni naimani Magu mtakuwa mmepiga asilimia 100 kwa awamu ya kwanza" anasema Mongella.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba,alisema vitambulisho hivyo vya awamu ya pili wamevipokea kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza vimegawiwa katika halmashauri 8 na Wilaya 7 za mkoa huo ikiwemo halmashauri ya Jiji la Mwanza wamepokea vitambulisho 20000,Ilemela 18000,Sengerema 6000,Buchosa 6000,Ukerewe 5000,Kwimba 6000,Misungwi 6000 na Magu 6000 .
Naye Kaimu Meneja wa TRA mkoa wa Mwanza Hoseya Kidasi anasema hii ni awamu nyingine ya kutoa vitambulisho ambapo tumekabidhi jumla ya vitambulisho 73,000 hivyo tunaunga mkono hatua zinazochukuliwa na Mkoa pia tutatatua changamoto ya mtandao ili kutoleta vikwazo na tutaongeza juhudi na kushirikiana ipasavyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba,anasema changamoto waliyokutana nayo ni wakati wakifanya ukaguzi wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao unakuta wamachinga wa eneo moja ambao wanavitambulisho wanaenda na eneo jingine,hivyo alitoa ushauri kuwa awamu nyingine vitambulisho viwekwe picha ya walengwa ili kuondoa changamoto hiyo.
"Biashara nyingi zipo mjini tunafanya matangazo ya gari ,na spika kwenye mitaa na tunatembea kuviuza kasi siyo nzuri tunachokiitaji ni kutumia nguvu kidogo " anasema Kibamba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.