Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuongeza kasi ili kukamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo .
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella baada ya kubaini kutokuwepo na ushirikiano na kasi ya ujenzi ikiwa ndogo huku akitoa agizo la kutaka kufikia Julai 3 majengo yawe yamesimama.
" Ikifika Ijumaa majengo hayajasimama patachimbika pia Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi ,Mhasibu na wengine mshirikiane na mfanye kazi kwa pamoja pia mtambue fedha hizo zinatumika ndani ya siku 90 hivyo ongezeni kasi",anasema Mongella.
Naye Kaimu Mhandisi wa Wilaya hiyo John Msonga akitoa taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo anasema ujenzi wa hospital hiyo unahusisha ujenzi wa majengo manne ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje(OPD) ,jengo la utawala, maabara na jengo la mionzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.