Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameuagiza uongozi wa kiwanda cha kusindika ngozi ghafi cha African tanneries kuhakikisha kinafanya kazi ndani ya miezi sita ijayo ili kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwa nchi ya Uchumi wa kati na yenye viwanda vitakavyotoa ajira kwa watanzania.
Mongella alitoa kauli hiyo mkoani hapa mara baada yakutembelea kiwanda hicho cha enzi za Hayati baba wa taifa na kukuta kimegeuzwa kuwa Ghala la kuhifadhia mitambo ya kampuni ya CASPIAN.
Sambamba na kuhakikisha kiwanda hicho kinafanyakazi, mkuu huyo wa mkoa ambaye yupo katika ziara za kukagua hali ya viwanda katika mkoa wake, pia ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanaondosha uchafu uliorundikana katika eneo la kiwanda hicho ndani ya siku kumi.
sambamba na, kuwasilisha ofisini kwake mpango kazi ifikapo Julai 20, 2017
“Kwa hiyo bwana mimi nakuelekeza tarehe 20 hiyo mabosi wako wawepo hapa, wakiwa na Mpango shughuli zinaanzaje hapa baada ya miezi 6”, alisema mongella na kuongeza kuwa ifikapo Januari 1, 2018 wakati wanasherekea mwaka mpya basi kiwanda hicho kiwe kimeanza kazi.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela ametoa muda wa miezi sita kwa uongozi wa kiwanda cha kusindika ngozi ghafi cha African tanneries kuhakikisha kuwa kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi mara moja badala ya kugeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia mitambo ya kampuni ya CASPIAN
Kiwanda hicho ambacho awali kilijulikana kama Mwanza Tanneries, kabla ya kubadilishwa jina kuwa African tanneries ni miongoni mwa viwanda vingi nchini vilivyobinafisishwa kwa wawekezaji wakati wa shughuli za ubinafshaji wa viwanda hapa nchini.
Mbali na kutembelea kiwanda hicho Mongella, pia alikagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu (flyover) unaoendelea katika eneo la Furahisha pamoja na awamu ya pili ya upanuzi wa barabara ya uwanja wa ndege utakaogharimu shilingi billioni tisa na millioni mia nne za kitanzania.
Mkuu wa mkoa wa mwanza yupo kwenye ziara ya kutembelea viwanda mbalimbali vilivyobinasfishwa na kushindwa kuendelezwa kwa mujibu wa makubaliano ya wawekezaji na serikali.
Mapema mwezi huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani hapa alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu huyo wa mkoa akimwelezea kuwa Mkoa wa mwanza umejipanga katika suala zima la mapinduzi ya viwanda na tayari kuna viwanda visivyo pungua 12 ambavyo vimeanza uzalishaji.
Kwa mujibu wa Bodi ya taifa takwimu mkoa wa Mwanza unaonesha unaviwanda vipatavyo1,470, huku viwanda vine vikiwa vimeajiri zaidi ya watu 500, saba vimeajiri watu kati ya 100 - 499, na viwanda vilivyo ajiri watu kati ya 50-99 vipo 8, viwanda vingine ni vile vilivyo ajiri kati ya watu 20-49 ambavyo idadi yake ni13, kwaupande wa viwnda vilivyo ajiri kati ya watu10-19 viwanda 22 na vile vilivyo ajiri kati watu ya 4-9 vikiwa ni viwanda 279 na mwisho kabisa ni viwanda vyenye watu kati ya 1-4 hivi jumla yake ni viwanda 1,074.
Mwanza ni mmoja ya mikoa inayokuwa kwa kasi huku uchumi wake ukichangia kwa asilimia 9% katika pato la taifa yaani GDP.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.