RC MTANDA AHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI YA GESI ILI KAYALINDA MAZINGIRA
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewakumbusha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya gesi badala ya mkaa ili kuendelea kuyalinda mazingira.
Akizungumza mapema leo asubuhi Januari 27,2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye Kijiji cha Mwisonge kata ya Idetetemya wilayani Misungwi wakati wa zoezi la upandaji miti 200 kusheherekea kumbukizi ya kuzaliwa ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, amebainisha kuwa matumizi ya mkaa ni tishio la ustawi wa mazingira na hewa ya ukaa.
"Leo tunasheherekea kumbukizi ya kuzaliwa ya Rais wetu kwa kumuunga mkono katika suala zima la utunzaji wa mazingira ambapo amesimama kidete kutuhimiza watanzania kutumia nishati ya gesi ili kuepuka ukataji wa miti ovyo," amesisitiza mkuu huyo wa wilaya.
Ameendelea kusema changamoto za tabia nchi na wingi wa hewa ya ukaa unatokana na kutozingatia utunzaji wa mazingira hivyo kuwataka wananchi kuupa kipaumbele kampeni ya mti wa mama kwa kupandi miti kwa wingi.
"Mkoa wetu wa Mwanza mwaka jana tulikuwa na kampeni ya kupanda miti milioni 12 lakini tumeishia milioni 7 sawa na asilimia 60,naamini tutaendelea kushirikiana kuhakikisha Mkoa huu unakuwa wa kijani,"Ludigija.
Kwa upande wake mhifadhi Mkuu kutoka Wakala wa huduma za misitu Kanda ya ziwa TFS,Benard Mwigulu amesema bado wanaendekea kutilia mkazo suala zima la elimu kuhusiana na faida ya upandaji miti kwa kuwashirikisha wanafunzi kama walivyo fanya leo kwenye shule ya Sekondari Mwisonge.
"Leo tumepanda miti ya Maparachichi na Miembe hii ni kumaanisha faida ya miti siyo kimvuli tu bali inawasaidia pia wanafunzi kupata lishe bora kwa kula matunda hali itakayowasaidia kufanya vizuri masomo yao,"Mwigulu.
Balozi wa mazingira nchini Mrisho Mabanzo amebainisha bado mkazo wa kuwahimiza jamii upandaji miti unatakiwa kutokana na zaidi ya asilimia 16 ya ardhi imekuwa ni jangwa.
Mkoa wa Mwanza katika kampeni ya Mti wa mama imepanda jumla ya miti 12000 katika Halmashauri zake 8.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.