RC MTANDA AIPONGEZA BONDE LA ZIWA VICTORIA KWA KUELIMISHA UMMA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza na kutoa maagizo kwa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kuhakikisha Jarida waliloliandaa kuhusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji jipya katika ziwa victoria (Salvinia Molesta) linawekwa katika mifumo mbalimbali ili jamii iweze kuona, kusoma na kusikiliza vizuri.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo mchana wa leo Mei 13, 2025 alipokuwa akizundua Jarida la Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria linalohusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji katika Ziwa Victoria ambapo amesisitiza umuhimu wa kuliweka jarida hilo katika mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa nakala mtandao.
Kadhalika Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa Bodi ya Bonde hilo kwa kuja na mpango wa jarida hilo kwa kuwa athari zinazotokana na Gugumaji hilo ni kubwa na inahatarisha uchumi wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
“53% ya Mkoa wa Mwanza umezungukwa na ziwa Victoria hivyo hapa Mwanza unapozungumzia maji unazungumzia uchumi, sekta ya usafirishaji, uhifadhi wa mazingira na wavuvi pia”.
kwa hiyo madhara ni makubwa sana na elimu hii mliyoitoa kupitia jarida hili ni muhimu sana kwa jamii na ninawapongeza sana kwa kazi kubwa iliyofanyika lakini bado ni endelevu na ni wajibu wetu kihakikisha kuwa ziwa victoria linaendelea kuwa safi. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Dkt. Renatus James Shinu amesema Jarida hilo ni maalumu na limelenga kuhakikisha taarifa muhimu ya shughuli, mbinu, na jitihada ambazo zimefanywa na Serikali katika kupambana na Gugumaji hilo ikiwemo na mipango ya baadae inawafikia Wananchi na Wadau wa sekta ya maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.