Mkuu wa Mkoa Mje. Said Mtanda leo Desemba 23, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (MB), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, katika ofisi yake, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya kijamii katika mkoa huo.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili mikakati ya kuimarisha ustawi wa jamii, hususan uwezeshaji wa wanawake, ulinzi na maendeleo ya makundi maalum pamoja na ushiriki wa jamii katika utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amempongeza Naibu Waziri kwa juhudi zinazofanywa na Wizara katika kusimamia agenda ya maendeleo jumuishi.

Kwa upande wake, Mhe. Naibu Waziri Mahundi ameeleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na viongozi wa mikoa na halmashauri ili kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi kwa ufanisi.

Aidha, Mheshimiwa Naibu Waziri ameanza ziara ya kikazi katika Wilaya za Ilemela na Nyamagana, ambapo anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali na kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa maeneo hayo kuhusu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya jamii.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.