RC MTANDA ALIVALIA NJUGA TATIZO LA USAFIRI ENEO LA KIVUKO CHA KIGONGO-BUSISI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amelazimika kuamuru mabasi na magari madogo kupita kwenye daraja la muda la mkandarasi eneo la Kigongo Busisi kutokana na kivuko cha MV Sengerema kuharibika injini na kusababisha hali ya uvukaji kuwa mgumu.
Akizungumza na wananchi eneo la kivuko leo Februari 2, 2025 wananchi waliokaa muda mrefu kusubiri kuvuka kuelekea Sengerema na mikoa ya Geita, Kigoma Kagera, Mtanda amesema tatizo hilo limesababishwa na hali mbaya ya magugu maji yaliyotapakaa ziwani humo na kusababisha uharibifu wa injini ya Mv Sengerema.
Amesema tayari amechukua hatua mbili,mosi amefanya mawasiliano na Wizara husika na masuala ya mazingira ili kuwaleta wataalam na wadau wengine wanaopambana na mazingira kuja kufanya utafiti wa kuyaondoa magugu maji hayo na pili amezungumza na Waziri wa Ujenzi ili alete injini mojawapo inayotarajiwa kufungwa kwenye vivuko vipya vitano vinavyojengwa hapa Mwanza.
"Poleni kwa usumbufu ndugu zangu wananchi tuwe na subira kidogo hali itatengemaa,tayari hatua za msingi nimefanya," amesisitiza mkuu huyo wa mkoa wakati anazungumza na wananchi hao.
Mtanda ambaye amelazimika kusimamia pande zote mbili Kigongo na Busisi upitaji wa magari hayo kwenye daraja la muda la mkandarasi,wasafiri hao walionesha furaha na kumshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa kuwakwamua baada ya kusota kwa saa nyingi kusubiri kuvuka.
"Nimekaa hapa kuanzia saa 8 mchana na sikuwa na matumaini ya kuvuka mapema na safari yangu ni Geita,tunamshukuru sana mkuu wa mkoa kwa kutupatia ofumbuzi," Richard Mahizo,msafiri
Kivuko cha Mv Sengerema kimesimama kutoa huduma hii ni wiki ya pili kutokana na injini yake kuharibika na kusalia vivuko viwili vinavyotoa huduma hata hivyo vimee lol elewa kutokana na idadi kubwa ya wasafiri na magari yanayopita eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.