RC MTANDA AMESEMA SERIKALI INA NIA NZURI YA KUFUNGA ZIWA ILI KURUHUSU UZALIANAJI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Serikali ina nia nzuri ya kulifunga ziwa viktoria kwa vipindi tofauti tofauti ikiwa na adhma ya kuruhusu uzalianaji na kuwafanya viumbe maji wawe wengi ili waweze kukidhi mahitaji ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza, Taifa na hata Kimataifa.
Aidha RC Mtanda amewataka wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi kuachana na uvuvi haramu kwani kwa kufanya hivyo kunapelekea kuadimika kwa kitoweo samaki.
"Uvuvi haramu unahatarisha usalama wa ziwa na viumbe maji vyote vilivyomo lakini pia unahatarisha hata usalama wa ajira za wananchi kupitia ziwa, ikitokea samaki wote wakaisha nina hakika hata wavuvi nao watakosa ajira". Amesema RC Mtanda.
Mhe. Mtanda ameyasema hayo mapema leo juni 07, 2024 alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Metro Fm kupitia kipindi cha Mambo mtelezo ambapo amesema Serikali ya Rais Samia imedhamiria kukomesha uvuvi haramu kwa kuwapatia wananchi mikopo ya boti na vizimba ili waweze kuvua kisasa na kuachana na uvuvi haramu.
Aidha Mhe. Mtanda pia amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuunda vikundi ili waweze kukidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo ya boti na vizimba vya kufugia samaki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.