RC MTANDA ARIDHISHWA NA UJENZI WA MIRADI YA KIMKAKATI MWANZA, AMSHUKURU RAIS SAMIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo ameendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi ya kimkakati akiwa wilayani Nyamagana ameanzia kuona ujenzi wa Soko kuu lililogharimu zaidi ya shs bilioni 23 na kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi ya miradi mbalimbali Mkoani humo, huku akimuhimiza mkandarasi Mohamed Builders kulikamilisha mapema.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua iliyofikia soko hilo ya 94% kabla ya kukamilika ni nzuri na tayari pesa iliyobaki shs bilioni tatu imeshatolewa na Serikali ili Mkandarasi akamilishe na wafanyabiashara waanze kufanya kazi.
"Tuendelee kumshukuru na kumuombea Rais wetu Samia Suluhu Hassan wakati anaingia madarakani soko hili lilikuwa hatua ya ujenzi asilimia 40 na Mkandarasi akiwa amelipwa 30%,lakini Rais akaongeza asilimia 60 ya malipo yake na sasa tunaona soko limebakiza asilimia 6 kabla ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi licha ya kupitia changamoto mbalimbali,asante sana Mhe.Rais,"Mkuu wa Mkoa.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu kutoka Halmashauri ya Jiji,Mussa Joram amebainisha soko hilo likikamilika wanatarajia kukusanya mapato ya shs bilioni 3.5 kwa mwaka.
Mkuu wa Mkoa akiwa kwenye mradi wa Hoteli ya nyota 5 inayojengwa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF wenye gharama ya sh bilioni 123 eneo la Capri Point,Mtanda amezihimiza Taasisi zote zinazohusika ikiwemo Tanesco na Mwauwasa kutoa ushirikano ili mradi huo uliofika asilimia 60 ya ujenzi ukamilike kama ulivyokusudiwa Disemba mwaka huu.
Mtanda amesema miradi kama hiyo inahitajika Mkoani humo kutokana na ujenzi wa uwanja wa ndege unaoendelea kufanyika ili uwe wa Kimataifa utaleta wageni wengi hasa watalii.
"Mhe Mkuu wa Mkoa Hoteli hii sasa hivi ipo asilimia 60 ya ujenzi,huduma kamili tunarajia kuanza kutoa Machi mwakani ikiwa na vyumba 195 vya kulala kikiwemo chenye hadhi ya Rais",Emmanuel Kahensa,Meneja NSSF Mwanza.
Mkuu huyo wa Mkoa alipofika kwenye mradi wa Meli ya Mv Mwanza inayojengwa eneo la Mwanza South amewapongeza Kampuni ya huduma za Meli MSCL kwa kuwa na chombo hicho cha kisasa na kinachoongoza kwa ukubwa ukanda huu wa Afrika eneo la maziwa.
"Huu ni mradi mkubwa sana ambao utachochea uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla,Mwanza ni Mkoa uliopo kimkakati eneo la nchi za maziwa makuu,Meli hii ikianza kutoa huduma kupitia nchi za Uganda na Kenya tutazidi kuimarika kiuchumi",Mkuu wa Mkoa
Amesema Meli hiyo itabeba abiria 1200 na tani ya mizigo 400 yakiwemo magari madogo 20 na Malori 3,ni huduma kubwa na ya kisasa ambayo Serikali imegharamia kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
"Meli hii imeigharimu Serikali shs bilioni 123 na Mkandarasi GAS ENTEC ameshalipwa fedha kwa asilimia 91 tunarajia mwishoni mwa mwezi huu tukabidhiwe Meli hii,"Erick Hamis,Mkurugenzi,MSCL
Mhe.Mtanda amekamilisha ziara yake siku ya leo kwa kukagua mradi wa chanzo cha maji eneo Butimba wenye gharama ya zaidi ya shs bilioni 71 na hapo amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maji na kuwataka wananchi kuilinda miundombinu ya rasilimali hiyo.
Mtanda amewakumbusha wananchi kujenga tabia ya kulipa ankara za maji kwa wakati ili Serikali izidi kupata fedha na kuwaongezea huduma bora.
"Hongera sana Nelly Msuya kwa hatua hii,mnatekeleza vizuri ilani ya CCM ya kumpatia huduma bora ya maji safi na salama mwananchi.
"Mhe.Mkuu wa Mkoa MWAUWASA tupo mbioni kujenga Matenki makubwa 5 yatakayokuwa na ujazo wa maji lita milioni 31 maeneo ya Fumagila,Buhongwa,Nyamazobe,Kisesa na Usagara lengo ni kuwapatia huduma endelevu ya maji wakazi wa maeneo hayo,"Nelly Msuya,Mkurugenzi MWAUWASA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.