RC MTANDA ASHIRIKI MAZISHI YA JAJI WEREMA KIAGATA - BUTIAMA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda leo Januari 04, 2024 ameshiriki mazishi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu Jaji Frederick Mwita Werema katika Kijiji cha Kongoto Wilayani Butiama Mkoani Mara huku akisema Serikali itaenzi na kukumbuka mchango wake
Mazishi hayo yameongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambapo amesema enzi za uhai wake Jaji Frederick Mwita Werema alisaidia kwa kiasi kikubwa katika utatuzi wa migogoro na kusema kuwa deni hilo limeachwa kwa watenda haki.
Jaji Werema alifariki tarehe 30 Desemba 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie, Apumzike kwa Amani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.