RC MTANDA ATAKA VITEKENDEA KAZI RUWASA VITUMIKE KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said
Mtanda amemtaka Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mwanza kutumia vitendea kazi vipya na vya kisasa vilivyotolewa kuboresha huduma za maji.
Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Novemba 06, 2024 wakati akikabidhi magari 4 na pikipiki 4 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 800 kwenye Ofisi za wakala huo Mkoa ambapo vitatumika kwenye ofisi za mameneja wa Wilaya za Kwimba, Sengerema na Misungwi.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha
wananchi wa vijijini wanapata huduma za maji safi kama wapatavyo kwenye maeneo ya miji na ndio maana wanaijengea uwezo RUWASA ili iweze kutekeleza miradi na kuwapatia wananchi huduma hiyo ni lazima watendaji wajitume.
Aidha, amebainisha kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani kumekua na ongezeko la hali ya usambazaji maji vijijini kwa asilimia 4 na ni shabaha ya Serikali kuona ifikapo mwaka 2025 wanafikisha asilimia 85 kwa wananchi wa vijijini kama ilani ya CCM ya 2020-25 ilivyosema.
Halikadhalika, amewapongeza RUWASA mkoa huo kwa kufikisha asilimia 72 kwenye usambazaji maji kwa wananchi ambao ni 65% ya wakazi wote na amewasihi kutekeleza vema miradi yote zaidi ya 50 inayoendelea inayogharimu zaidi ya bilioni 146.
Meneja wa RUWASA Mkoa huo Godfrey Sanga ameishukuru Serikali kwa vitendea kazi hivyo na ameahidi kuvitumia kama ilivyokusudiwa na kwa hakika vitakwenda kuongeza huduma kwani vitasaidia kuifikia miradi katika usimamizi.
Aidha, amebainisha kuwa hapo awali walikua wanatumia fedha zaidi ya milioni 300 kukarabati magari chakavu 6 waliyokuwa nayo katika wilaya zote na kwamba kwa sasa ofisi imepata ahueni kwa kupata magari nadhifu na ya kisasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.