RC MTANDA ATOA SOMO KWA MAAFISA USAFIRISHAJI MWANZA
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji Bw.Peter kasele amewataka Maafisa wasafirishaji wa mizigo na abiria mkoani Mwanza kufuata sheria za Ushirika.
Amesema hayo leo february 26, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Victoria Palace katika hafla ya kukabidhi vyeti vya ushirika kwa kundi hilo (UWAMWA) kutoka ofisi ya Mrajisi ya Mkoa.
“Rai yangu kwa UWAMWA nawahimiza kuzingatia sheria na kanuni za Ushirika na sheria zingine za nchi, wataofanya ubadhirifu na kusababisha hasara katika vyama hivi hatua kali za zitachukuliwa dhidi yao”. Amesema Kasele.
Amezungumzia pia dhima ya Serikali katika kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na Wizara ya mifugo na uvuvi na benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania ili kuinua uchumi na kijamii kwa wanachama.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Mwanza Ndg. Leo Zephania amewapongeza viongozi waanzilishi kwa kazi nzuri waliofanya hadi kufanikisha usajili wa chama chao,amewataka viongozi waliochaguliwa kuzingatia sheria ya vyama vya Ushirika Na 6 ya mwaka 2023 na sheria nyingine za nchi katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha amewashauri kuzitumia Ofisi za Ushirika wilaya na Mkoa kwa ushauri wa masuala ya uendeshaji wa chama chao,na pia amesisitiza suala la ushirikiano ndani ya chama pamoja na wadau wengine wa maendeleo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa shughuli za chama.
Naye, mwakilishi wa mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini ( LATRA) Bi. Maria Chacha ameweka wazi dhamira na matarajio ya kufikisha huduma kwa 90% kidigitali mpaka 2026.
Vilevile, ameomba ushirikiano kwa wadau na madereva wote wa vyombo vya usafiri huku akiahidi Ushirika umekuja na jawabu la kuwapatia madereva mikataba ya kazi ili kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi na uaminifu kwa sababu hapo mwanzo hapakuwa na mikataba jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa migogoro mingi na kuibiwa kwa vyombo vingi vya usafiri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.