• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AWAALIKA WALIOKOSA ELIMU RASMI KUJIUNGA NA MPANGO WA ELIMU WATU WAZIMA

Posted on: September 15th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa wito kwa wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 ambao  wamekosa elimu ndani ya mfumo rasmi kutumia fursa ya uwepo wa vituo vya elimu ya watu wazima kupata maarifa na ujuzi.

Ametoa wito huo mapema leo tarehe 15 Septemba, 2025 akiwa katika uwanja wa Sabasaba Wilayani Magu kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la Elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Mkoa wa Mwanza.

Amesema, Mkoa huo una zaidi ya watu 2625000 ambao hawajui kusoma na kuandika na kwamba serikali imeanzisha vituo katika Halmashauri zote nane ambapo kuna zaidi ya wanafunzi elfu 36 wanaopatiwa elimu nje ya mfumo rasmi hivyo mi fursa ya kukimbilia kwa wote waliokosa.

Mhe. Mtanda amebainisha kuwa elimu ya watu wazima inajumuisha programu mbalimbali ikiwemo MEMKWA ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuwawezesha waliokosa elimu ya msingi kupata stadi za kujua Kusoma, kuhesabu na kuandika ili kufuta ujinga.

Aidha, amebainisha kuwa ndani ya mfumo huo kipo kipengele cha MUKEJA ambacho kinatoa fursa ya kutoa maarifa kwa uwiano ambapo jamii inapewa stadi za ujuzi mbalimbali za ujasiriamali na akabainisha kuwa kuna zaidi ya wafungwa 300 mkoani humo wanapatiwa elimu hiyo.

Vilevile, ametumia wasaa huo kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa kwa vijana walioodolewa kwenye mfumo rasmi kwa sababu mbalimbali kama mimba, kupata tena nafasi ya kusoma na kutimiza malengo yao.

Akitoa taarifa ya Mkoa Dkt. Onesmo Nyamweru amesema juma jilo linaadhimishwa kila mwaka jirani na tarehe 8 septemba kwakua ndiyo siku ya Kisomo cha Kimataifa ulimwenguni kote na kwamba maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kutafakari dhana na maendeleo ya Programu za elimu ya watu wazima kupitia maendeleo ya teknolojia.

“Elimu nje ya mfumo rasmi kitaifa imepanda kutoka 78% hadi 83% na kwa Mwanza wanaojua kusoma na kuandika ni 85.6% elimu hii ni nyenzo muhimu ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi na inakidhi mahitaji ya watu wazima ya sasa kwa jamii iliyo katika shughuli za uzalishaji mali.” Amesema Dkt. Nyamweru.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA AWAALIKA WALIOKOSA ELIMU RASMI KUJIUNGA NA MPANGO WA ELIMU WATU WAZIMA

    September 15, 2025
  • RC MTANDA AWATAKIA HERI BENCHI LA UFUNDI PAMBA JIJI FC MSIMU MPYA

    September 12, 2025
  • MAAFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI WAASWA KUSIMAMIA MISINGI YA KAZI

    September 12, 2025
  • RC MTANDA AKABIDHI MAGARI YA BILIONI 1.3 KWA JESHI LA POLISI

    September 12, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.