RC MTANDA AWAHAKIKISHIA WANA MWANZA USALAMA WA VIVUKO
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema usalama wa vivuko vinavyofanya kazi zake za usafirishaji katika Wilaya ya Ukerewe, Sengerema na Misungwi ni salama na hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani wamekuwa wakivifuatilia na kuvikakagua mara kwa mara na endapo dosari inapodhirika wamekuwa wakivifanyia ukarabati wa haraka.
Mhe. Mtanda ameyasema hayo leo tarehe 07 juni, 2024 wakati alipokuwa akifanya mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha runinga cha Star Tv kupitia kipindi cha Tuongee Asubuhi ambapo amesema changamoto za vivuko vyote Mkoani Mwanza zimeshatatuliwa na sasa vivuko vyote ni salama.
Aidha Mhe. Mtanda amesema kwa sasa Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujengaji wa vivuko vinne vya kisasa vinavyojengwa na Mtanzania ajulikanaye kama Songoro Marine ambapo kivuko kilicho chini kabisa kiko 70% na cha juu zaidi kiko 95%.
"Mara baada ya ukamilishaji wa ujenzi wa vivuko hivi, changamoto ya uhaba wa vivuko kwa Mkoa wa Mwanza tutakuwa tumeimaliza na hiyo ndio adhma ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Mtanda anaendelea na ziara yake ya kutembelea na kuzungumza vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kuyasemea yale yote yaliyofanywa na Serikali ikiwemo dira ya Mkoa wa Mwanza katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.