RC MTANDA AWAPOKEA WAJUMBE KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI Z'BAR.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Novemba 18, 2024 amewapokea wajumbe kutoka Baraza la wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao ni wajumbe wa kamati ya huduma ya ustawi wa jamii na kuonesha imani kile walichokuja kujifunza kitaongeza maendeleo kwa wananchi wanao wawakilisha.
Akizungumza na ujumbe huo Ofisini kwake, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha Mwanza kuna miradi mingi ya afya hivyo watapata fursa nzuri ya kujifunza namna inayotekelezwa na pia namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
"Hii ni ziara muhimu sana,maana kamati yenu inagusa maisha ya watu kwa upande wa afya, hapa Mwanza tuna jumla ya wilaya saba kunakotekelezwa miradi mingi ya afya,naamini mtakachojifunza mtakwenda kuishauri kwa hekima Wizara ya afya na hatimaye kuwepo na tija kwa wananchi",Mtanda alipokuwa akitoa taarifa fupi ya Mkoa wa Mwanza kwa wajumbe wa Baraza la wawakilishi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Sabiha Filfil Thani amesema ziara yao ya siku nne mkoani Mwanza watapata mengi ya kujifunza na kwenda kuishauri Serikali ili kuboresha zaidi sekta ya afya.
Mganda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Jesica Lebba amesema kufanya vizuri katika miradi mingi ya afya inayoletwa na Serikali ya awamu ya sita mkoani Mwanza kumechangiwa na wajumbe hao wa Baraza la wawakilishi kuja mkoani humo kupata nafasi ya kujifunza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.