RC MTANDA AWATAKA BODABODA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka maafisa usafirishaji wa pikipiki za abiria (Bodaboda) Mkoani humo kufuata sheria za usalama wa barabarani ili kujiepusha wao na abiria wanaowabeba na ajali za barabarani.
Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Novemba 09 2024 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza wakati akifungua Mkutano mkuu wa jumuiya hiyo ambapo wanakwenda kuchagua viongozi katika ngazi za kanda, mkoa na wilaya wa kundi hilo.
"Nawasihi sana twendeni tushirikiane kuzuia ajali, tutambue kwanza kuwa hatuvai kofia ngumu (helmet)kwa ajili ya kumfurahisha askari wa barabarani (trafiki) bali ni kwa faida yetu wenyewe." Mhe. Mtanda.
Aidha, amewataka kuwa walinzi wa amani baina yao kwa kuhakikisha kila mmoja anamfahamu mwenzake na anapoona mwenendo mbaya unaoashiria uhalifu basi mara moja atoe taarifa katika uongozi wa serikali ya mtaa.
Ametumia wasaa huo kuwataka pia kuacha tabia za kuchagua viongozi ambao ni wababe na wabishi kwa ajili ya kuwaandaa kubishana na viongozi wa wilaya bali wakachague viongozi waadilifu ili wawasaidie siku za usoni.
"Twendenu tukashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya jumatano Novemba 27, 2024 na pia tunaimarishe usalama katika kipindi chote cha uchaguzi huu." Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Mhe. Mtanda ameichangia jumuiya hiyo inayoendesha shughuli zao na kaulimbiu isemayo 'Bodaboda Usafiri Salama' Tshs. 500,000 kwa ajili ya kuwaongezea nguvu katika majukumu yao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.