RC MTANDA AWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA ELIMU YA WATU WAZIMA KUJIELIMISHA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wananchi waliokosa elimu ndani ya mfumo rasmi kujielimisha kupitia fursa zitolewazo na mpango wa elimu ya watu wazima ili kupata uelewa.
Ametoa agizo hilo leo Septemba 6, 2024 katika viwanja vya Mirongo Jijini Mwanza wakati akihitimisha juma la elimu ya watu wazima lililoadhimishwa kwa wataalam wa elimu kutembelea vituo vya kutolea elimu na ufundi stadi ndani ya Mkoa huo.
"Tungetamani kuona wana Mwanza na Watanzania wote waliokosa elimu kwenye mfumo rasmi wanapata elimu hiyo kupitia elimu ya watu wazima ili kuondoa ombwe la wananchi wenye elimu na waliokosa ili kuwa na usawa." Mkuu wa Mkoa.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa watu wazima kwa mchango wa ujenzi wa jamii zetu hivyo nawapongeza Wizara ya Elimu kwa usimamizi.
" Serikali inatambua mchango wa elimu ya watu wazima katika kupanua, kuimarisha na kuendesha huduma ya upatikanaji wa elimu kupitia fursa mbalimbali zilizopo". Mkuu wa Mkoa
Naye Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Kusirie Swai ametoa rai kwa Magereza nyingine mkoani humo kuiga mfumo wa Magereza ya Butimba kwa kutoa elimu kwa wafungwa wanaoingia gerezani na kuwapatia ujuzi.
Juma hilo la wiki ya Elimu ya watu wazima limeadhimishwa kuanzia Septemba 4, 2024 na kuhitimishwa leo Septemba 6, 2024 chini ya kaulimbiu isemayo "Ujumuishaji wa Elimu Bila Kikomo kwa Ujuzi Ustahimilivu Amani na Maendeleo".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.