Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mlezi wa Timu ya Pamba Jiji, Mhe. Said Mtanda leo Septemba 12, 2025 amewatakia heri timu ya pamba jiji katika safari ya kuanza msimu mpya wa mashindano ya ligi kuu.
Mkuu wa Mkoa amewataka wachezaji kwenda kucheza kwa bidii huku wakiitanguliza Mwanza mbele kwa kuwa sasa sio timu ya Halmashauri ya Jiji pekee bali ni timu ya Mkoa.
"Sisi tunataka nafasi ya juu, nendeni mkapambane, sisi tumetimiza wajibu wetu ni jukumu lenu pia kutuheshimisha".
Kadhalia Mhe. Mtanda ametoa rai kwa wachezaji hao kuzingatia nidhamu mchezoni na hata nje ya uwanja na kamati ya maadili haitamvumilia mchezaji yoyote atakaekwenda kinyume na sheria zilizowekwa.
Kabla ya kuhitimisha salamu zake kwa benchi la ufundi Mkuu wa Mkoa amesema jukumu lake kama Mlezi wa Timu hiyo ni kuhakikisha timu inapata wadhamini wengi na kuwatosha ili iweze kusonga mbele bila vizuizi.
Timu hiyo ya Pamba Jiji inatarajia kuondoka Jumamosi tarehe 13, Septemba kuelekea Mkoani Lindi kwenda kuanza msimu kwa kukichapa na timu ya Namungo katika uwanja wa CCM Majaliwa (Ruangwa) Septemba 18, 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.