Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi wakizingatia sheria za usajiri wa mashirika yao na kuhakikisha wanalinda maadili, mila na silka za nchi.
Ametoa agizo hilo mapema leo julai 25, 2025 wakati akizungumza na Mashirika yasiyo ya Kiserikali zaidi ya 150 waliokutana katika Jukwaa la Mwaka la mashirika yasiyo ya Kiserikali kujadili utekelezaji wa kazi.
Amesema ni vibaya kwa mashirika hayo yaliyoaminiwa na kusajiriwa kuingia kwenye mtego wa kuharibu mila za nchi kwa maslahi tu ya kupata fedha bali wanapaswa kwa pamoja kulinda maadili ya nchi.
“Msipokee fedha tu ili kujinufaisha, tekelezaeni majukumu yenu na mtoe taarifa kwa mamlaka zinazowasimamia na hakikisheni mnalinda mila na desturi za kitanzania kwani taifa letu linajipambanua kitaifa na kimataifa kwa amani na maadili mema.” Mhe. Mtanda.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu, Mhe. Mtanda ameyataka mashirika yaliyopata nafasi ya kufanya uangalizi kufuata sheria za Tume Huru ya Uchaguzi.
“Usalama wetu ni kitu muhimu, nchi ikiharibika, amani ikitoweka sisi ni waathirika wa kwanza, ni heri kuwa masikini kwenye nchi yenye amani kuliko kuwa matajiri katika mazingira yasiyo salama”, amesisitiza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.