RC MTANDA KUZUNGUMZA NA WIZARA KUCHAGIZA UJENZI WA BARABARA MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema ofisi yake itaandika barua kwenda wizara ya ujenzi kukumbushia utekelezaji wa barabara katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambazo zimekwama kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo leo tarehe 20 Desemba, 2024 wakati wa kikao cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2024/25 kilichoketi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Mhe. Mtanda amesema kuna barabara kadhaa zimekwama kukamilika Mkoani humo kutokana na sababu mbalimbali hususani malipo ya wakandarasi na ukamilishi wa taratibu za usanifu hivyo ni wakati sasa kwa ofisi yake kuwaandikia barua kufuatilia kwa karibu ujenzi huo.
Akitolea mfano wa barabara zinazotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kama Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Sengerema - Nyehunge yenye urefu wa zaidi ya Kilomita 50 ni kwamba imekwama kwa zaidi ya miaka 2 sasa.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ambrose Pascal amesema Mtandao wa barabara za Mwanza ni muhimu sana hususani kwa uchumi wa wafugaji na wakulima hivyo serikali inajitahidi kwa kadiri ya upatikanaji wa bajeti kuhakikisha zinajengwa na kukarabatiwa.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kununua hati fungani ya uwekezaji wa miundombinu ya barabara (Samia Bond) inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kukusanya fedha ili zitekelezwe barabara zinazosimamiwa na TARURA kwa kipindi cha miaka mitano ambapo mnunuzi anapata riba ya asilimia 12 kwa mwaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.