Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel ameadhimisha siku ya Wauguzi Duniani akiwataka wakina mama wajawazito kuzingatia kanuni zote za afya ili kulinda afya zao na mtoto.
Akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika ki-Mkoa kituo cha Afya Buzuruga Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza,Mhe Gabriel amesema Afya ya mama na mtoto itaimarika kwa kuzingatia kufika vituoni ambapo huko atapata tiba sahihi na ushauri wa kitaalam.
"Mama zangu nimefurahi kuwaona hapa natambua leo ni siku yenu ya kuja kupata matibabu na maendeleo ya afya zenu,zingatieni sana lishe bora kuepuka Utapiamlo"
Akiwa kituo cha Afya Buzuruga Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea kuona shughuli mbalimbali za Wauguzi na kuwakumbusha kuzingatia viapo vyao katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema Wauguzi ndiyo uti wa mgongo katka Sekta ya Afya hivyo amewakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia viapo vyao wakati Serikali ikiendelea kuzifanyia kazi changamoto za mazingira yao ya kazi.
Naye Makamu wa Rais wa Chama cha Wauguzi nchini TANNA, Ibrahim Mgoo ameiomba Serikali kuendelea kuwekeza kwa Wauguzi kwa kuwajengea uwezo ikiwemo kuwaendeleza kitaaluma.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Mwanza,Martha Mkinga amesema bado muuguzi mmoja anawahudumia wateja kuanzia 20 hadi 30 badala ya 6 hadi 8 wanaendelea kuamini Serikali itaifanyia kazi changamoto hiyo.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani Kitaifa yamefanyika Mei 22 mwaka huu Mkoani Kilimanjaro kauli mbiu yake ikiwa ni WAUGUZI SAUTI INAYOONGOZA WEKEZA KWENYE UUGUZI NA HESHIMU HAKI KULINDA AFYA KWA WOTE.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.