Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel ameahidi kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari katika kuuletea Maendeleo Mkoa huo.
Mhe Gabriel amesema hayo katika hafla ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo ki-Mkoa yamefanyika Juni 3 Jijini Mwanza na kusisitiza Vyombo vya Habari ni nguzo muhimu nchini katika kuelimisha,kuhabarisha na kuburudisha.
"Mwanza ni Mkoa wa Kimkakati tuna Miradi mingi yenye lengo la kuwaletea Maendeleo Wananchi hivyo mchango wa Vyombo vya Habari hapo unahitajika ili Umma ujue kinachoendelea kwa faida yao" Mkuu wa Mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewakumbusha Waandishi wa Habari kutokubali kuyumbishwa na wachache wenye maslahi yao binafsi badala yake kuzingatia misingi ya Taaluma yao.
"Kalamu yenu ni muhimu sana ikienda tofauti madhara yake ni makubwa angalieni wenyewe baadhi ya machafuko yaliyotokea na yanayojiri sasa kwa baadhi ya Mataifa mengine yamechangiwa na Wananchi kupotoshwa na kuzua ghasia" amesema Mhe Gabriel.
Katika hafla hiyo Mhe Gabriel pia amezindua Akaunti Maalum ya Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza,MPC iliyopo Benki ya Mkombozi kwa lengo la kuchangia ujenzi wa Ofisi ya Chama hicho.
Mwenyejiti wa Chama cha Waandishi Mwanza,Edwin Soko amesema kwa muda wa miaka mitatu wamekuwa wakifanya Maadhimisho hayo Kanda ya Ziwa na yamekuwa na faida kubwa kutokana kupata wasaa wa kukutana na Wadau mbalimbali na kujenga mshikamano wa pamoja.
Amesema mkakati uliopo sasa ni kuyafanyia Maadhimisho hayo Kitaifa na kuweka sasa mkazo katika kuutangaza Mkoa wa Mwanza katika Sekta zote vikiwemo vivutio vyake vya kitalii.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yamefanyika Kitaifa Mei 27 Mkoani Arusha na Mwanza walilazimika kuyasogeza mbele hadi Juni 3 kuyapisha ya Kitaifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.