Mkoa wa Mwanza umepanga kuhakikisha inatoa chanjo kwa watoto 846,733 na imejipanga katika vituo 355 ambapo jumla ya watoa huduma 6,909 wamepata mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel leo Mei 18,2022 alipokuwa akizindua Chanjo ya matone ya Polio katika kituo cha Afya Nakatunguru kilichopo Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
"Ukerewe ina jumla ya wakazi 518,114 kati yao watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ni 108,937 ambao ndiyo lengo la chanjo ya Matone ya Polio," amesema Mhandisi Robert Gabriel.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema,tulizoea kufanya shughuli hizi za uzinduzi makao makuu ya Mkoa na kuahidi kuwa ni mwanzo wa kufanya Shughuli za kimkoa na nyingine zitaendelea kufanyika Wilayani hapa.
"Kampeni hii itafanyika kwa siku 4 kuanzia tarehe 18 hadi 21 Mei 2022 ambapo lengo ni kuchanja watoto 846,733 katika Mkoa Mzima kwa Wilaya ya Ukerewe inatakiwa kuchanja watoto 108,937."
Dkt.Rutachunzibwa ameongeza kuwa Chanjo zitatolewa kupitia vituo 355 vikiwemo vituo 38 vya Wilaya ya Ukerewe na Watoa huduma 6,909 wamepata mafunzo kwa ajili ya kazi ya Uchanjaji,Watunza takwimu na wahamasishaji.
"Tumesambaza chanjo Dozi 973,740 katika vituo vyote na maandalizi ya kutoa chanjo hiyo yamekamilika na chanjo hii inatolewa bila malipo.
Naye Diwani wa kata ya Nakatunguru,Mataba Sosthenes ameshukuru kwa uzinduzi wa kampeni ya Polio katika kata yao na amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel kuwasadia katika maboresho ya huduma mbalimbali katika kituo cha afya cha Nakatunguru.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.