Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel amezindua rasmi msimu wa ununuzi wa zao la Pamba 2022/2023 Kijiji cha Mahaha Wilayani Magu na kutangaza bei elekezi ni Shilingi 1560.
Akizindua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Johari Samizi amesema Serikali bado inaendelea kumpigania Mkulima kuhakikisha ana neemeka na jasho lake.
"Tuna dhamira ya dhati ya kumkomboa Mkulima,bei ya Pamba msimu uliopita ilikuwa Shilingi elfu moja na hamsini na msimu huu mmeona mabadiliko."
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Anthony Diallo amesema nia ya Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kila Mkulima anafanya kazi yake katika mazingira mwafaka bila kudhulumiwa na walanguzi wa mazao
Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amebainisha wamejipanga kuongeza kasi ya kusimamia na kuratibu uzalishaji wa zao la Pamba.
Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri amesema ataendelea kuzungukia Mikoa yote inayolima zao hilo kumuelimisha Mkulima namna ya kufaidika na Pamba.
Mkoa wa Mwanza unatarajia kuvuna tani 2000 za Pamba msimu huu na Serikali inaendelea kumjengea uwezo Mkulima ili aweze kuvuna tani Milioni moja mwaka 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.