Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba pamoja na timu yake ya usimamizi wa huduma za afya mkoa (RHMT) leo Oktoba 22, 2025 wamefanya usimamizi shirikishi kwenye maeneo na vitengo mbalimbali katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando.
Akizungumza katika ufuatiaji huo Dkt. Lebba amesema ziara hiyo imelenga pia kupata mrejesho katika maeneo yanayofanya vizuri na maeneo yenyechangamoto kutoka kwa wakurugenzi wasaidizi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ili kuona namna ya kuboresha.

Aidha ameongeza kuwa ziara hiyo itaisaidia ofisi yake kubaini mambo ambayo yanarudisha nyuma huduma za haraka kwa wagonjwa wa rufaa ambapo amesema atalishughulikia akishirikiana na timu za usimamizi wa huduma za afya za Halmashauri (CHMT) ambapo wagonjwa wengi wa rufaa ndiko wanakoanzia matibabu.
“Ziara yetu inamafanikio sababu pamoja na mambo mengine tumebaini kwamba kwa kipindi cha miaka mitano ufuatiaji wa nanmna hii haujawahi kufanyika na tumebaini moja ya sehemu ya kuboresha ni kukuhakikisha wagonjwa wa rufaa wanafika kwa wakati ili kuondokana na vifo.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.