RMO MWANZA AFUNGUA MAFUNZO YA KIKANDA YA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amefungua mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya
Ebola, Maburg, Mpox Ebola na cholera jijini Mwanza yaliyolenga kuweka uthibiti wa maambukizi na uzuiaji wa magonjwa ya milipuko.
Ufunguzi huo umefanyika mapema leo Machi 4, 2025 katika ukumbi wa Gold crest ambapo walihudhulia wadau mbalimbali kutoka ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile Tanzania, Kenya, Uganga,Rwanda, Sudan kusini na wawakilishi kutoka Ujerumani.
Dkt. Lebba amewataka washiriki kutumia mafunzo hayo kama njia ya kuimarisha mifumo na kulinda jamii dhidi ya magonjwa tishio, huku akiweka wazi umuhimu wa kutumia mifumo hiyo katika jamii.
”sote tunafahamu madhara ya milipuko ya hivi karibuni nchini Congo, Uganda, Rwanda, hata hapa Tanzania, hivyo lazima tuendelee kuwekeza katika mafunzo ili kudhibiti maambukizi ya kinga (IPC) na matumizi sahihi ya vifaa ya kujikingia (PPE)”. Amesema Dkt. Lebba.
Kwa upande wake Dr. Eric Nzeyimana ambaye ni mkuu wa idara ya Afya ya EAC amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuimarisha usalama katika ukanda wa afrika mashariki.
Aidha, ameweka wazi juhudi za kuendelea kujifunza kutokana na milipuko ya awali ili kuboresha mwitikio kwa siku zijazo na akawataka wahudumu wa afya kukabiliana na changamoto hizo kwa ujasiri na ujuzi wa kutosha.
Naye, Mheshimiwa Bw. Edouard Nkuzimana kutoka katika kitengo cha Uandaaji na Ujibuji wa Dharura, Afrika amewataka watu kutoa taarifa kwa wakati pale ambapo wahapohisi dalili kwa kuzingatia usalama wa raia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.