RMO MWANZA APOKEA TELEVISHENI 57, KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA KWENYE VITUO VYA AFYA
Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa amepokea Televisheni 57 Kutoka Wizara ya afya kwa lengo la kutoa taarifa na kusaidia utoaji wa huduma bora kwenye vituo vya afya mkoani humo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Februari 07, 2024 kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa ukiwakutanisha Wawakilishi kutoka Wizara hiyo, TAMISEMI na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
"Tunategemea kuwa hizi televisheni zitaeneza ujumbe ambazo wagonjwa pamoja na watumiaji wa vituo vyetu watakuwa wanavifuatilia wakipata mafunzo mbalimbali kutoka kwenye mada mbalimbali ambazo zinahusiana na masuala ya afya" Mganga Mkuu.
Dkt. Rutachunzibwa ametumia wasaa huo kuwataka wananchi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari za kuepukana na Ugonjwa hatari wa Kipindupindu.
Mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jaina Msuya amesema lengo la Mradi huo ni kupeleka umeme kwenye vituo vya afya na pampu za maji vijijini ambao unafikia vituo vya afya 57 nchi mzima pamoja na pampu za maji 363 ambazo zimesambaa kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa gharama ya mradi ni billion 37.4.
"Lengo la kuanzisha huu mradi ni kuwawezesha wananchi wanaokaa maeneo ya vijijini waweze kupata huduma kwa haraka na muda sahihi." Amefafanua.
Pia amewataka wananchi kutumia maji ambayo ni safi na salama yawasaidie katika matumizi yao ya kila siku kwa sababu yatawasaidia kuwalinda na kutunza afya zao, na itapunguza kero ya kutafuta maji kwa umbali mrefu hasa kina mama na kuweza kupata muda wa kushiriki kwenye majukumuu mengine kama ya kifamilia.
Mwakilishii kutoka Wizara ya afya James Mhilu ameishukuru wakala wa nishati vijijini (REA) pia ameongeza kwa kuelezea namna gani mradi huo unaenda kuwasaidia wananchi moja kwa moja, uhakika wa maji na vituo vya kutolea huduma za afya kupata umeme na kuhakikisha kuwa huduma ya chanzo itaimarika ili kuweza kupambana na magojwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuwataka watu wazingatie unawaji wa mikono kwa maji safi na sabuni ili kuepukana na magonjwa, lakini pia mradi huu unaenda kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika vituo vya afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.