Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya na baadhi ya wataalamu kutoka Mkoani wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo Wilaya ya Sengerema.
Akiwa kijiji cha Nyasenga kata ya Nyampande Mhe.Mongella ametembelea mradi wa maji ambao amekuta unaendea na ujenzi na kuwahakikishia kuwa ifikapo januari 2020 Nyasenga itakuwa na maji.
"Mradi huu hadi kukamilika utahudumia kijiji cha Kawekamo,Nyampande na Nyasenga ambapo wakazi zaidi ya elfu 10 tunategemea wapate maji,"alisema Mongella.
Naye Diwani wa kata ya Nyampande Mhe.George Kazungu amesema vifaa vipo na kazi inaendelea na kuwaasa wananchi waendelee kuwa na subira wakati kasi ikiendelea kuongezwa.
Hata hivyo mbali na miradi ya maji inayotekelezwa na MWAUWASA Mhe.Mongella alikagua ujenzi na upanuzi wa Zahanati ya Kaseenyi iliyopata Shilingi milioni 10 kutoka kwa Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli Julai 5,2017 na kukuta ujenzi unaendelea.
Aidha Mhe.Mongella amekagua ukarabati mkubwa wa kituo cha Afya Kagunga na ujenzi wa chuma cha kujifungulia Zahanati za Ngoma A na Mtimba inayofadhiliwa na "Aga Khan Development Network" ambapo alipata fursa ya kuhutubia wananchi na kuwahamasisha kujiandikisha katika daftari la wapiga kula ili walishiri uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.