SERIKALI IMETOA BILIONI 31.5 UJENZI WA KITUO CHA KULEA VIPAJI VYA MICHEZO MALYA: RC MTANDA
Rai imetolewa kwa wanamichezo kuendelea kuzichangamkia fursa mbalimbali kwenye sekta hiyo kutokana na Serikali kuzidi kuboresha miundombinu kwa ujenzi wa kituo kipya cha kulea vipaji vya michezo chenye gharama ya shs bilioni 31.5 kinachojengwa katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo MALYA.
Akizindua jioni hii mbio za Transec Lake Victoria Marathon, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amesema jitihada za Serikali ya awamu ya sita ya kuboresha sekta ya michezo ina lengo la kuhakikisha tunakuwa na wanamichezo bora.
"Niwapongeze waandaaji wa mbio hizi zenye lengo la kuutangaza utalii ndani ya ziwa Victoria,ni dhahiri mnamuunga mkono kwa vitendo Rais wetu ambaye ameonesha nia ya kuinua michezo hapa nchini," Mkuu wa Mkoa
Amesema sekta ya Utalii ina mchango wa asilimia 17 katika pato la Taifa,na Mwanza imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo havina budi kutangazwa kwa njia mbalimbali.
"Tumeshuhudia Rais wetu akiutangaza utalii wetu kupitia filamu ya Royal Tour na sasa idadi kubwa ya watalii wanakuja nchini,naamini tukizidi na sisi kutangaza vivutio vilivyopo hapa tutapokea watalii wengi,"RC Mtanda.
Mratibu wa mbio hizo Halima Chake amesema huu ni mwaka wa nne wanaofanya mashindano hayo ambayo yamezidi kuwa na mwamko kwa Jamii
"Mhe.Mkuu wa Mkoa tumepanga sehemu ya mapato kupitia mbio hizi kuwanunulia taulo za kike wasichana 500 waishio katika mazingira magumu wilayani Ukerewe"Mratibu
Mbio hizo zitakazo anza kutimua vumbi Juni 30 mwaka huu ni za km 2.5 zitakazo wahusu watoto chini ya miaka 10,km 5 mshiriki yoyote, na km 10 hadi 21 kwa wale wazoefu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.