Wilaya ya Magu itaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa kuongezewa mingine kumi mwaka huu ukiwemo ujenzi wa madarasa manne na Maabara moja kwenye shule ya Sekondari Igekemaja ambayo bado haijaanza rasmi.
Akizungumza na wananchi Wilayani Magu kwenye Vijiji vya Ihayabuyagu na Igekemaja alivyovitembelea kukagua miradi ya TASAF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama amesema Serikali ipo imara kuharakisha maendeleo ya wananchi wake hivyo ni wajibu kwa viongozi kuisimamia kikamilifu.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa miradi inayotekelezwa na TASAF fedha zake zinaletwa mapema kwenye Halmashauri hivyo anataka kuona miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
"Nimekagua nyumba hizi za Watumishi wa afya hapa Ihayabuyaga sijaridhishwa na kutokamilika mapema hadi leo wakati fedha zimeletwa tangu Aprili mwaka jana,hii yote itachangia kuwacheleweshea Wananchi maendeleo".Waziri Mhagama.
"Tunatambua umuhimu wa miradi hii ya TASAF inavyo leta mageuzi chanya kwa wanachi,tunakuahidi Mhe.Waziri kuifuatilia ili kujiridhisha inaendelea kuwa na tija kwa wanufaika"Joachim Otaru kaimu Katibu Tawala Mkoa
*Mhe Waziri tunamshukuru Mhe.Rais kwa kutujali watu wa Magu TASAF imetoa Shs milioni 103 kwa ujenzi wa nyumba hizi za Watumishi wa afya na madarasa mawili Sekondari ya Igekemaja zimetolewa Shs milioni 64,tunaendelea kumuunga mkono kwa vitendo ikiwemo kuwashirikisha wananchi ujenzi wa Kituo cha afya hapa Ihayabuyaga"Rachael Kasanda Mkuu wa Wilaya ya Magu.
"Kutujengea madarasa haya mawili kupitia mradi wa TASAF kwenye shule hii ya Igekemaja,hali hii imezidi kutuongezea ari sisi wananchi kuendelea kuchangia nguvu zetu ili kuikamilisha haraka na watoto wetu waanze masomo haraka" Mhe.Deusdery Kiswaha Mbunge wa Magu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.