Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amekabidhi Magari pamoja na Vifaa vya Uokozi kwa Jeshi la Zimamoto na na Uokozi Mkoani humo na akatumia wasaa huo kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha jeshi hilo.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi vifaa na magari hayo sita iliyofanyika leo tarehe 21 Oktoba, 2025 katika viwanja vya ofisi ya jeshi hilo Jijini Mwanza Mhe. Mtanda amesema serikali inaonesha kwa vitendo kiu ya kumaliza changamoto za uokozi kwa haraka hivyo jeshi hilo lina wajibu na dhamana ya kuvitunza vifaa hivyo.

"Tufuate kanuni na taratibu za jeshi letu kuhakikisha magari na vifaa hivi vinafanya kazi zilizokusudiwa na si vinginevyo, madereva na wasimamizi wa vyombo hivi wahakikishe wanavitunza vizuriā.

Amesema, miaka ya nyuma jeshi hilo halikuaminika na wananchi kwa kuchelewa kwenye majanga hususani ya moto lakini kwa sasa serikali inahakikisha inaboresha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.