Serikali imewahakikishia stahiki zao za fidia kulipwa kwa usahihi na mapema Wananchi wa Vijiji vya Sotta na Nyabila vilivyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ambao wanafanyiwa tathmini ya mali zao kupisha shughuli za Mgodi wa Madini.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dktr Angelina Mabula akiongozana na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali amefanya mkutano wa hadhara kuzungumza na Wananchi hao baada ya baadhi yao kushindwa kupata ufahamu sahihi dhidi ya maeneo hayo na zoezi la tathmini kwa ujumla.
Mhe Mabula amesema kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 97 hakuna mtu anayeweza kumiliki maeneo ya Milima,Maziwa,Mito au sehemu za Bahari hivyo ni vyema Wananchi watambue ili kuepusha migogoro isiyo na tija.
"Nimelazimika kuja kuwapa ufafanuzi huu na kuwaondolea shaka baadhi yenu katika zoezi zima la fidia ambalo kabla Mtathmini Mkuu wa Serikali,Everyn Magasha amelikamisha na hekari moja mtalipwa Shilingi Milioni 2 ikiwa ni nyongeza kutoka Milioni 1.5 ambayo ndiyo bei ya soko la radhi hii" Mhe Mabula.
Amesema Serikali ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kupigania kuinua Uchumi wa Nchi na Mwananchi imeweka mazingira mazuri kwa Wawekezaji wanaokuja hivyo kazi iliyopo ni kumpa nafasi Mwekezaji huyo aanze kazi mapema iwezekanavyo.
Naibu Waziri wa Madini Dktr Steven Kiruswa amesema tayari Serikali imeshaingia mkataba na Mwekezaji huyo ambaye tayari ametumia Shilingi Bilioni 240 kwa shughuli za Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa yaliyomo ndani ya Mkataba huo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amesema hii ni fursa nyingine ya kuwainua kiuchumi Wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo wajibu wao sasa ni kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni Mmbia na Mwekezaji huyo.
Asilimia 85 tayari wameshiriki zoezi la kufanyiwa tathmini ya mali zao kabla ya kulipwa fidia huku asilimia 15 wakiwa bado kutokana na kutopata ufahamu wa kuhusu fidia zao ambapo sasa wamesha elimishwa na wanatarajiwa kuthaminishwa maeneo yao.
Fidia nyingine watakazo lipwa Wananchi hao ni pamoja na Nyumba,Makaburi,Mazao stahiki,Posho ya kusafirisha mizigo tani 12, na Posho ya miezi 36 ya kujiandaa na makazi mapya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.