SERIKALI YAZINDUA NDEGE NYUKI KUIMARISHA DORIA ZIWA VICTORIA
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mara ya kwanza imenunua na kuzindua matumizi ya ndege nyuki (drone) itakayofanya kazi ya kuimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi katika Ziwa Victoria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ndege nyuki hiyo Rock Beach Hotel wilayani Nyamagana leo Aprili 13, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Alexander Mnyeti amesema Serikali imeamua kuchukua hatua madhubuti za kisasa kuhakikisha inadhibiti uvuvi haramu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Mhe. Mnyeti ameongeza kuwa katika awamu hii wizara imetumia kiasi cha Shilingi Milioni 259, kwa ajili ya ununuzi wa ndege nyuki, kutoa mafunzo kwa waendeshaji, kufunga vituo vya kudhibiti, kufanya usajili na kuanzisha mfumo wa kuhifadhi na kuchambua taarifa zinazopatikana kutoka kwenye ndege hiyo.
“Ndege nyuki hii ni kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi katika Ziwa Victoria. Ndege nyuki hii ina uwezo wa kukimbia kwa mwendo kasi wa Kilometa 108 kwa saa na uwezo wa kuchukua picha za matukio kutoka umbali mita 350 na kuruka mita 120 kutoka usawa wa bahari na kusafiri umbali wa Kilometa 400 na kuweza kukaa angani kwa muda wa saa mbili.” amesema Mhe. Mnyeti
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.