Kikao cha wadau wa michezo kimefanyika mapema hii leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, lengo la kujadili maandalizi ya Bonanza la michezo lililoandaliwa na shirikisho la michezo la mashirika ya Umma Taasisi na makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililopangwa kufanyika tarehe Octoba 12 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa michezo Mkoa wa Mwanza, James William amesema kama mkoa wa Mwanza umeyakubali mashindano haya ya Bonanza kwani yatafungua mlango wa michezo kwa mashirika, viwanda na makampuni pia itakuwa na faida kwa wafanyakazi.
“Sisi Mkoa wa Mwanza tumeyakubali na tukasema uwe mlango wa michezo kwa mashirika, viwanda na makampuni na zipo faida za kuwa na michezo kwa wafanyakazi kama kujenga afya kutokomeza baadhi ya magonjwa kama magojwa ya moyo na kisukari,” Alisema William.
Aidha, William amesema kuwa bonanza hilo la michezo limepokelewa kama moja wapo ya fursa ya kujenga mahusiano nakukuza uchumi katika mkoa wa Mwanza.
“Ninaamini wageni wataokuja katika kushiriki katika bonanza hili watafanya hoteli zipate watu, vituo vya petrol vitapata watu na mwisho wa siku mzunguko wa uchumi utakuwa umepatikana Mwanza.’’Alisema William.
Naye mwenyekiti wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma taasisi na makampuni binafsi Tanzania,(SHIMMUTA), Khamis Mkanach amebainisha kuwa bonanza hilo litahusisha michezo mbali mbali na kuomba mashirika mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki..
‘’Bonanza hili la michezo litajumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu,mchezo wa kuvuta kamba ,mchezo wa kufukuza kuku, mchezo wa bao, mchezo wa karata pamoja na mchezo wa draft.’’Alisema Mkanach.
Hata hivyo, Mkanach ameweza kuweka wazi kuwa zitakuwepo zawadi mbali mbali kwa wale watakaoibuka washindi katika bonanza hilo la michezo.
‘’wataoibuka washindi katika bonanza hilo watapata zawadi mbali mbali zikiwemo medali,vikombe pamoja na zawadi ya mpira kwa mchezaji atayefunga hat trick katika mchezo wa miguu’’.Alisema Mkanach
Pamoja na hayo Mkanach ametoa wito kwa wadau hao kuweza kutangaza bonanza hilo, pia ameweza kutoa wito kwa makampuni mbali mbali kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika bonanza hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.