Zaidi ya wakazi 2000 kutoka Wilaya ya Nyamagana na maeneo jirani mkoani Mwanza wamepatiwa huduma mbalimbali za kitabibu zinazo husisha vipimo vya macho na meno,bila gharama zozote kupitia shirika la Compassion Conect kutokea nchini Marekani.
Akijiridhisha na utolewaji wa huduma hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel anasema serikali inatoa pongezi kwa shirika hili ambalo limejitwika moja kwa moja jukumu la kujali afya za wananchi.
anaongeza kuwa wameleta vitu,vifaa kwa ajili ya kufanya hilo zoezi na wamesema wako tayari kuhakikisha kama tunamahitaji mengine ya pamoja wapo tayari katika kutusaidia kuona namna gani tunaweza kuwahudumia wananchi katika maeneo hayo pia serikali itaendelea kushirikiana na Shirika hilo .
Kwa upande wake Afisa Muunguzi kutoka Shirika la Compassion Connect Robert Renatus anaeleza kuwa
shirika hilo lenye makao makuu nchini marekani na limefanikisha hatua hii ya kutoa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na maradhi tofauti.
Anasema mwananchi wamejitokeza kwa wingi lakini baadhi ya matatizo yaliyojitokeza na kuchangia kukwamisha uharaka wa zoezi hilo baada ya mwaamko mkubwa ni watu kukwepa huduma zinazotolewa na madaktari wenye asili ya kitanzania.
"Mtu anatamani angalau akiguswa na mzungu mambo yanakuwa vizuri kuhusu ilo mchungaji alihakikisha kila chumba ambacho kinahudumia wagojwa angalau kuwe na mzungu mmoja na mwafrika mmoja kwa kiasi hicho tumefanikiwa kuhakikisha wagonjwa wanarizika na huduma zetu" anaeleza
Anaongea kuwa Matibabu ya shinikizo la damu, meno na macho ni miongoni mwa huduma kuu zilizotolewa na shirika la hilo ambayo yamedumu kwa wiki moja huku idadi kubwa ya walioshiriki wakitajwa kubainika na matatizo ya macho.
Ezekiel Lupima na Getruda Richard ni baadha ya wananchi walionufaika na huduma hizo za viwango na zisizo na malipo walieleza kuwa walikabiliwa na tatizo la macho kwa kipindi kirefu hivyo huduma walizopatiwa imekuwa ni mwanga katika maisha yao na walitoa shukrani zao kwa shirika hilo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.