SIDO KUWENI MSTARI WA MBELE KUWAINUA WAJASIRIAMALI: RC MTANDA
Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) limepewa Rai ya kuwa mstari wa mbele kuwainua Wajasiriamali wa Mwanza ili wawe wazalishaji bora watakao inua uchumi wa Mkoa huo.
Akifungua wiki ya Ubunifu kwenye ukumbi wa Rock City Mall ambayo inasheherekewa Duniani kote leo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema SIDO ina wajibu wa kuhakikisha Wajasiriamali wanazidi kubadilika na kupiga hatua hadi ngazi ya kimataifa.
"Nimejionea shughuli zenu, hongereni sasa msiridhike na hatua hiyo ongezeni bidii ili mfike hatua ya kulimudu soko la Kimataifa." Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa SIDO ina wataalamu na uwezo wa hali ya juu ya kuwainua Wajasiriamali hao kupambana na umasikini kwa bidhaa zao kuwa na ubora na kuondokana na dhana potofu kuwa kila kizuri ni kutoka nje ya Tanzania.
"Epukeni kujihusisha na Taasisi za kijanja ambazo zimetapakaa sehemu nyingi zitakazo ishia kula jasho lenu na kuishia kufaidika wao,"
Wiki hiyo ya Ubunifu inayokwenda kwa siku tatu imeambatana na Makongamano na maonesho ya bidhaa mbalimbali kwenye viwanja vya Rock City Mall.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.