SIMAMIENI KIKAMILIFU AFUA ZA LISHE BORA SHULENI: AFISA ELIMU MKOA
Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Martine Nkwabi amewataka wasimamizi wa afua za Lishe kutoka shule za Msingi na Sekondari kusimamia zoezi la utoaji elimu bora ya Lishe kwa vijana balehe na jamii nzima kuona umuhimu wake kwa vijana hao.
Akizungumza leo Agosti 9, 2024 katika mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu hao kwenye ukumbi wa mikutano Nyakahoja, Nkwabi amewashukuru walimu hao kwa mwitikio mzuri na kuwahimiza kutorudi nyuma katika kufanikisha zoezi hilo na mwishowe liwe na tija kwa Taifa.
"Tanzania ina takribani robo ya idadi ya watu wake wakiwa ni vijana balehe, ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za lishe kama utapiamlo, upungufu wa vitamini na madini, pamoja na uzito uliopitiliza, hali hii inaathiri ustawi wa kimwili, utendaji wa kiakili, na uwezo wa vijana kufaulu masomo na kujenga afya bora kwa maisha yao ya baadaye,"Nkwabi.
Aidha, amelishukuru Shirika la Nutrition International pamoja na Taasisi nyingine zisizo za Kiserikali kwa mchango wao wa kuboresha sekta ya afya.
Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha afua za lishe nchini ili kupunguza matatizo yanayotokana na lishe duni na kuhakikisha afya bora kwa vijana wa Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.