Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu(SUMATRA) imefanya mkutano kati yao na wamiliki wa magari pamoja na madereva wa magari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, kwa ajiri ya kutatua changamoto za usafirishaji wa barabarani na kutoa elimu ya maombi ya leseni kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bw.Gilliad Ngewe amesema kuwa kazi ya SUMATRA ni kusimamia huduma za usafirishaji wa barabara na majini kwa kufuata sheria,kanuni na utaratibu na kutoa elimu ili kuondoa umiliki wa leseni feki na wasio na leseni na kuwaondoa vishoka.
"Tutadhibiti mitandao yote feki ya jutoaji leseni,rushwa na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wamiliki wote wa leseni feki, pia kwa kuwafungia vifaa maalum vya kudhibiti mwendo kwenye mabasi ya mikoani, kwa ajili ya kuzuia ajari za barabarani, ili kusaidia kupunguza matumizi makubwa ya mafuta, matumizi ya matairi mabovu na ufungaji wa breki njiani ovyo,"alisema Ngewe.
Kwa upande wake Meneja wa leseni SUMATRA Leo Ngowi ameeleza jinsi ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kusema kuwa vitu vinavyohitajika kwenye kujaza maombi ya kwa njia ya mtandao ni lazima uwe na Nakala ya kadi ya udereva, Bima ya gari, Nakala ya leseni ya Udereva na Hati ya ukaguzi, kwa kutumia njia hii itasaidia kuondoa leseni feki na kuokoa muda.
Nao wamiliki na madereva wa magari wametoa changamoto zao hasa katika upande wa faini za mara kwa mara za barabarani, kuondoa vishoka, na kuzingatia upande wa walemavu, wawe wanakuja wenyewe SUMATRA barabarani kukagua na kuomba matatizo hayo yarekebishwe na sio kuendelea kuongelewa kila siku bila kufanyiwa marekebisho.
Aidha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Issa Hamad ameekezea juu ya ukaguzi wa leseni na bima kwa njia ya mtandao.
"Endapo akiingiza namba ya bima na leseni yako kama ni feki au imeisha muda wake mfumo huwa unasema na matokeo yake unatakiwa kwenda kulipa faini pia muda mwingine tunakukagua gari lako pasipo kukuambia ila tukigundua kama unakosa huwa tunakulipisha faini na kukupa risiti ukalipie kwa kukwepa malumbano ya kuanza kukuelezea kosa tutachukua mda mrefu,"alisema Hamad.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza ACP M.K. Mkadam amesema anahitaji wampelekee magari ya polisi yanayofanya makosa, anahitaji watendaji wake wafanye kazi na ametoa namba ya simu kwa wananchi kwa ajiri ya kuwashitaki madereva ambao hawafikishi katika vituo wanavyohitaji kushuka, na alisisitiza kutoa elimu zaidi ili waende na wakati.
Hata hivyo Mhe.Ngewe amemalizia kwa kuwataka madereva na wamiliki wa magari wafuate sheria, kanuni na utii ili kuondoa matatizo ya barabarani na waache kutoa rushwa hivyo itasaidia kuondoa leseni feki na vishoka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.